
FAHAMU BIASHARA 19 ZA KUANZA NA MTAJI MDOGO ZENYE FAIDA Tuangalie biashara 19 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000(laki moja) unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa. Hakuna biashara ndogo, ila kuna biashara unazoweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa. Hiyo ambayo inaitwa “biashara ndogo” ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku itakutoa. Kabla hatujaenda kwenye hiyo orodha ya hizo biashara za mtaji mdogo, hebu tuweke sawa kauli ya “zenye faida kubwa”. Faida kubwa haimaanishi mamilioni ya fedha, bali ni kwamba faida utakayoipata kulingana na mtaji wako ni nzuri na usipokata tamaa itakufikisha mbali. ZINGATIA: Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile, ni vyema kufuatilia utaratibu na sheria za mahali ulipo. Tafadhali ilinde biashara yako kwa kufuata kanuni zote zilizowekwa na serikali. Baada ya kulisawazisha hilo, twende kwenye hiyo orodha ya biashara za mtaji md...