Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya benki

VIGEZO 8 VINAVYOTUMIWA NA TAASISI ZA KIFEDHA KUKUPA MKOPO WA BIASHARA

Picha
Kupata mkopo kutoka kwa taasisi za fedha ni hatua muhimu kwa wajasiriamali wengi wanaotaka kuendeleza biashara zao.  Hata hivyo, taasisi hizi zina vigezo maalum wanavyotumia ili kuhakikisha kuwa wanakopesha kwa watu au biashara zinazoweza kurudisha mikopo hiyo kwa wakati.  Kujua vigezo hivi ni muhimu ili uweze kujiandaa vizuri na kuongeza nafasi zako za kupata mkopo. Hapa chini, tutaelezea kwa undani vigezo hivi na kutoa mifano ya jinsi unavyoweza kukidhi mahitaji haya. TAZAMA VIGEZO HAPA CHINI  1.Historia ya Mikopo (Credit History)    -  Taasisi za fedha huangalia historia yako ya mikopo ili kujua kama umekuwa ukilipa mikopo yako ya awali kwa wakati. Hii inawasaidia kutathmini hatari ya kukukopesha.    - Mfano :  Ikiwa umewahi kukopa kutoka benki na ukalipa kwa wakati, hii itaongeza nafasi zako za kupata mkopo mpya.  Kinyume chake, ikiwa una historia ya kuchelewa kulipa mikopo, inaweza kuwa vigumu kupata mkopo. 2.Mpango wa Biashara (Bus...

MAMBO 7 YA KUZINGATIA KABLA HUJAFANYA MAAMUZI YA KUCHUKUA MKOPO WA BIASHARA BENKI

Picha
Kuchukua mkopo kwa ajili ya biashara ni hatua kubwa inayohitaji umakini na maandalizi mazuri. Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuchukua mkopo kutoka kwenye taasisi ya fedha: 1 . Sababu za Msingi za Kukopa    - Hakikisha una sababu maalum na za msingi za kuchukua mkopo. Usikope kwa sababu tu una fursa ya kukopa, bali kwa sababu una mpango mzuri wa jinsi utakavyotumia fedha hizo kuongeza uzalishaji au mauzo katika biashara yako. Mfano: Fikiria unamiliki duka la vifaa vya ujenzi huko hapo ulipo.  Unaona fursa ya kuongeza bidhaa mpya kama mabomba na vifaa vya umeme ambavyo vina mahitaji makubwa.  Kukopa fedha ili kuongeza bidhaa hizi kunaweza kuongeza mauzo yako na faida. Hii ni sababu nzuri ya kukopa kwani una mpango maalum wa jinsi utakavyotumia fedha hizo kuongeza uzalishaji. 2. Uzoefu na Ujuzi katika Biashara    - Ni muhimu kuwa na uzoefu na ujuzi wa kutosha katika biashara unayokusudia kuendeleza kwa mkopo. Kukopa ili kuanzisha biashara mpya...

SABABU 10 ZINAZOFANYA BIASHARA NYINGI ZINAZOANZISHWA TANZANIA KUFA

Picha
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha biashara nyingi zinazoanzishwa kufa, hasa katika mazingira ya Tanzania.  Hapa kuna maelezo ya kina kuhusu baadhi ya sababu hizo na sababu ya mwisho imechangia biashara nyingi zaidi kufa. 1. Mipango Duni ya Biashara Biashara nyingi zinaanzishwa bila mipango madhubuti. Mpango wa biashara unapaswa kujumuisha malengo, mikakati ya masoko, muundo wa utawala, na makadirio ya kifedha.  Kwa mfano, mfanyabiashara anayeanzisha duka la nguo bila kujua wateja wake walengwa ni akina nani na jinsi ya kuwafikia, anaweza kushindwa kupata wateja wa kutosha. 2. Uongozi na Usimamizi Mbaya:  Uongozi bora ni muhimu kwa mafanikio ya biashara. Biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya uongozi mbovu na usimamizi duni.  Kwa mfano, kampuni inayoshindwa kusimamia vizuri rasilimali zake, kama vile wafanyakazi na fedha, inaweza kupata hasara na hatimaye kufa. 3. Kutowajali Wateja:   Wateja ni msingi wa biashara yoyote. Biashara nyingi zinakufa kwa sabab...

UKIWA MGENI KWENYE BIASHARA USIKIMBILIE KUWINDA WATEJA FANYA HILI KWANZA

Picha
Imekua ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wapya kwenye biashara fulani kufikiria kupata mauzo mengi mwanzoni wakati wanaanza. Wengi wanakua na matarajio makubwa ya kuuza na huvyo muda na nguvu nyingi wanatumia kusaka na kuwinda wateja. Badala ya kutumia muda mwingi na nguvu katika  kutengenenza thamani na kujenga jina la biashara yake kwanza. Unakuta mfanyabiashara ni mpya kabisa kwenye biashara lakini anakua na matarajio makubwa au afanane idadi ya wateja na wenzie walio na miaka mitano kwenye biashara hiyo hiyo. Mfano wewe unafanya biashara yako kwa kutangaza bidhaa au huduma zako mtandaoni na hapo ulipo una wafuasi(followers) elfu moja unataka ufanane na mwenzio alie na followers elfu 10. Ukiwa na matarajio makubwa yatakufanya upaniki pale ambapo utakua hupati wateja. Cha msingi cha kufanya kwanza inabidi ujenge jina ili ujulikane kwanza na vile vile ujifunze namna ya kujenga thamani ya huduma au bidhaa unayouza. Ukiwa kama wale wafanyabiashara wanaopenda shortcut kwenye bi...
Picha
 MAMBO MATANO (5) YA KUZINGATIA KABLA YA KUCHUKUA MKOPO WA BIASHARA BENKI Kabla ya kuchukua mkopo wa biashara toka taasisi ya fedha au taasisi binafsi ni muhimu ukafanya uchambuzi yakinifu juu ya mkopo husika. Kumbuka mikopo huwa inatolewa kwa masharti kadhaa ikiwemo kuuzwa kwa dhamana ulizoweka kwa ajili ya kulinda mkopo husika.  Hivyo elewa kabisa kama umechukua mkopo bila kuelewa misingi ya namna bora ya matumizi ya mkopo inaweza ikakuletea changamoto baadae. 1.KUWA NA LENGO LA MKOPO Ni muhimu kuwa na kuelewa hasa unahitaji mkopo kwa ajili ya lengo lipi,au unachukua tu mkopo kwasababu umesikia kuna sehemu wanatoa mikopo kiwepesi nawe unaenda kuchukua. Je lengo la kuchukua mkopo ni kwa ajili ya kuwekeza kwenye nini kwenye hiyo biashara yako.  Epuka kuchukua mkopo wa biashara lakini unachepusha kupeleka kwenye matumizi mengine nje ya lengo la mkopo Weka pesa ya mkopo kwenye biashara kama lengo husika ulivyopanga alafu matumizi yako binafsi yatoke kwenye faida utakayopata...