
JUA NAMNA TANO (5) YA KUUZA KWA KUTEKA HISIA ZA MTEJA Hivi umewahi nunua kitu wakati ukiwa na furaha sana halafu baadae ukajikuta unajutia maamuzi ya manunuzi yako? Au yale maamuzi ya kitu fulani ulinunua kwasababu ya uwoga tu uliokua nao kwa kuogopa labda kile kitu kitaisha,ukajikuta unanunua haraka haraka. Halafu siku zinaenda unakuta kile ulichonunua hakina manufaa au kinaendelea kuwepo lakini wewe uliogopa ukajua baadae huenda kitaisha dukani n.k Hizo ni baadhi ya hisia ambazo huwa zinawakuta watu na hujikuta wakifanya maamuzi kwa kuendeshwa na hisia badala ya fikra za kimantiki(logic). Kuuza kwa kuzingatia hisia alizonazo mteja ni jambo la msingi kuliko hata huduma au bidhaa yako ilivyo. Kwani huwa inaaminika kuwa watu huwa wananunua vitu/huduma kutokana na hisia watakazopata kutoka kwenye hiyo huduma/bidhaa kuliko hata,namna bidhaa au huduma hiyo ilivyo. Hii kwa maana nyingine ni kuwa watu huwa wananunua kutokana na namna watakavyojisikia wakiwa na kitu ulichowau...