
UMUHIMU WA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA BIASHARA YAKO Biashara nyingi huporomoka au nyingine hufa kabisa kutokana na kutokuwepo kwa mikakati bora ya ufuatiliaji mwenendo wa biashara husika. Watu wengi hujikuta wamefanya matumizi makubwa mpaka wanajikuta wametumia na mtaji wa biashara. Hii husababishwa na uzembe wa kutotunza kumbukumbu au taarifa za mapato yanayoingia na matumizi. Biashara yoyote ili iweze kufanikiwa,utunzaji wa kumbukumbu ni nguzo muhimu sana. Kuna msemo huwa unasema “mali bila daftari huisha bila habari” NI KWANINI WATU HAWATUNZI KUMBUKUMBU ZA BIASHARA? Kuna sababu kadhaa ambazo huwa zinafanya watu waone shida kutunza kumbukumbu za biashara,tutaziangalia baadhi yake hapa chini. KUKOSA ELIMU YA KIBIASHARA Watu wengi huanzisha biashara kabla au pasipo kupata elimu ya kutosha kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia katika ufanyaji biashara. Na mojawapo ya elimu hizi ni pamoja na elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara. Hivyo hujikuta wakipot...