Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya pesa
Picha
ZINGATIA HATUA HIZI 6 ILI UFIKIE UHURU WAKO WA  KIFEDHA KIURAHISI Kila mmoja huwa ana ndoto fulani ya kuwa siku moja awe na pesa nyingi ili aweze kutimiza mahitaji mbalimbali. Lakini huwezi kufikia uhuru huo wa kifedha kama endapo hutachukua hatua kadhaa sasa. Tumeelezea baadhi ya hatua sita(6) ambazo ukizichukua zitakufanya uepukane na suala la kuhangaika na uhaba wa kifedha mara kwa mara. 1. FUTA MADENI YENYE RIBA KUBWA Moja ya kitu kinachomaliza pesa zako ni madeni yenye riba kubwa.  Ni kweli mkopo sio mbaya lakini pale ambapo unachukua mikopo yenye riba kubwa sana huwa inaumiza. Kumbuka riba ni gharama ya mkopo uliochukua,lakini kama endapo utakua na mikopo mingi yenye riba kubwa jua kiasi kikubwa cha pesa utakua unatumia kulipa riba za mikopo, na kuwafaidisha waliokupa mkopo,hivyo kuwa makini kwenye hili. 2.PUNGUZA MATUMIZI YASIYO NA ULAZIMA Anza sasa kujifanyia tathimini juu ya matumizi yako kwenye vitu unavyopenda kununua. Jilulize je hiki kitu kina umuhimu kwa sasa,au ...