Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya mtandaoni
Picha
MAKOSA 6 YATAKAYOFANYA AKAUNTI YAKO YA WASAP IFUNGWE  Haya ndio makosa 6 ukiyafanya yanaweza sababisha akaunti yako ya WhatsApp izuiwe au kufungwa kabisa kutumika. 1. KUTUMIA TOLEO LISILO RASMI LA WHATSAPP  Hapa ni kwa wewe unaependa kutumia App ambazo sio rasmi kwa ajili ya WhatsApp. Hapa tunamaanisha Apps kama WhatsApp GB au WhatsApp Plus,itafanya akaunti yako kufungwa. Kwani WhatsApp hawataki utumie toleo lisilo rasmi,hivyo achana na hizo WhatsApp GB na matoleo mengine ya hovyo. 2.KUTUMA VITISHO AU MAUDHUI MABAYA Kutuma ujumbe wa vitisho au kudhihaki wengine au kufanya watu wawe na hofu. Ukifanya matendo haya kwa muda mrefu utakuja kukuta akaunti yako ya WhatsApp imezuiwa kufanya kazi,hivyo kuwa makini na ujumbe wa kutishia watu. 3.UKIRIPOTIWA MARA KWA MARA NA WATU Kama endapo utakuwa unaripotiwa mara nyingi na watu basi jua muda sio mrefu akaunti yako itafungwa. Hivyo tumia WhatsApp kiustaarabu na kiusalama ili watu wasitume report kuwa unawakera. 4.KUUNGA WATU KWENYE MAGR...
Picha
PROMOTE BIASHARA YAKO SASA KWENYE MTANDAO WA X (TWITTER) Mtandao wa X(zamani Tweeter) umekua ni mtandao unaotumiwa na watu wengi kwa sasa. Kuanza kufikiria namna ya kupromote biashara yako kwa kupitia matangazo ya kulipia kwenye mtandao huu ni jambo la muhimu. Kama ilivyo mitandao mingine kama vile Instagram,Facebook,Tikok na mtandao wa X nao unazo huduma za kupromote matangazo ya biashara yako. Kwa kuweka utaratibu mzuri wa kibajeti na kuwa na malengo yako ya kibiashara ni rahisi zaidi kuwafikia mamilioni ya watu waliopo kwenye mtandao wa X. VIGEZO VYAKE NI VIPI? Ili uweze kufanya matangazo ya kulipia katika mtandao wa X ni lazima uwe na akaunti ya mtandao wa X ambayo umeifanya kuwa ni ya biashara(professional account). Akaunti ya biashara inapatikana kwa kuibadilisha akaunti yako hiyo ya kawaida na kuipeleka iwe ya biashara kwa process ndogo kwenye App hiyo hiyo. Kuifanya akaunti kuwa ya biashara(professional account) ni sharti la muhimu kama ilivyo katika mitandao mingine kama Insta...
Picha
 MAMBO 8 YA KUFANYA ILI USITAPELIWE MTANDAONI Matapeli mtandaoni wameongeza spidi ya kutapeli watu. Nawe inabidi ujue namna ya kuchukua tahadhari ili usitapeliwe. 1.USIFANYE MALIPO HARAKA HARAKA Hata kama umeona bidhaa au huduma inakuvutia kwa mara ya kwanza hasa kwa mtu usiemfahamu usikimbilie kulipia haraka  Jipe muda huenda ni hisia zako za tamaa zinakufosi ulipie kwa sasa. Kumbuka matapeli wana lugha ya kuvutia sana. 2.KUWA MAKINI NA VITU AU HUDUMA ZA BEI NDOGO SANA Kuna wale watu wanatangaza wanauza vitu au huduma kwa BEI ndogo sana. Hadi unajiuliza anapataje faida? Kuwa makini matapeli huwa wanaweka vitu bei ndogo ili kukuvutia ili ukilipia tu basi humpati tena. 3.FANYA UTAFITI KUHUSU TAARIFA ZA MHUSIKA Kabla hujalipia bidhaa au huduma kwa mtu usiemfahamu ni vizuri kufanya utafiti kwanza. Angalia mawasiliano yake,anapatikana wapi, na vitu vingine vingi. Mara nyingi matapeli taarifa zao huwa zimejificha ficha hazieleweki,ukijaribu kumpigia simu au video call hapokei au h...