JUA FAIDA ZA KUFANYA UWEKEZAJI KWENYE HISA ZA MAKAMPUNI

Mfanyabiashara na tajiri mkubwa Duniani Warren Buffett ambaye ni muwekezaji mkubwa aliwahi kusema “ kama hutajifunza namna ya kutengenenza fedha ukiwa umelala,jua utaendelea kufanya kazi mpaka kifo chako kikukute” . Pointi ya msingi ya Warren Buffett ilikua ni msisitizo juu ya umuhimu wa kufanya uwekezaji ambao unaweza kukuingizia mapato hata bila uwepo wako(passive income). Yaani umefanya uwekezaji watu wengine au system zinaendelea kukuingizia kipato bila hata wewe kuwepo eneo husika. Fikiria umefanya uwekezaji halafu mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka pesa inaingia tu kwenye akaunti yako bila wewe kutumia nguvu kubwa na muda. Katika andiko hili tutaelezea aina mojawapo ya uwekezaji ambao unaweza kukuingizia mapato bila uwepo wako ingawa inahitaji nguvu na jitihada kubwa mwanzoni wakati wa kuwekeza. Tutaangalia nini maana,faida,na ugumu wa kuwekeza kwenye Hisa za makampuni. Na vilevile tutaona ni mambo gani ya msingi ya kuzingatia kabla hujawekeza katika Hisa. NINI MAANA YA HISA...