Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya matumizi
Picha
MAENEO 10 YA KUPUNGUZA MATUMIZI YAKO ILI USEVU PESA NYINGI  Kukata au kupunguza matumizi katika maeneo kadhaa ni mkakati muhimu ambao utakusaidia kuwa na ziada ya pesa kwa ajili ya matumizi mengine muhimu ya kimaendeleo. Tunaangazia maeneo 10 ambayo ukiyazingatia itakusaidia kuwa na kiasi kikubwa cha pesa kinachobakia 1. PUNGUZA MATUMIZI YA KODI YA NYUMBA NA BILI -Pango la nyumba Kama wewe umepanga ni vizuri kuishi nyumba ya gharama nafuu inayoendana na kipato chako ili kupunguza gharama za kulipa kodi kubwa na mwisho wa siku unajikuta pesa yako nyingi inaishia kulipa kodi. Fanya utafiti wa sehemu ambako unaweza kupata nyumba nzuri lakini kwa gharama ya chini ili upunguze gharama za pango. -Bili za umeme na maji Punguza matumizi ya gharama za umeme na maji kwa kuwa na mikakati mbalimbali kama kuzima taa pale ambapo hazitumiki na kutotumia maji hovyo ili kupunguza gharama za umeme na maji. 2. PUNGUZA MATUMIZI YA VYAKULA Chakula ni hitaji la muhimu ambalo kila binadamu anahitaji,na k...