Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya masoko

NJIA 10 ZA KUDHIBITI WAFANYAKAZI WAKO ILI WASIKUIBIE KWENYE BIASHARA YAKO

Picha
Katika ulimwengu wa biashara, uaminifu wa wafanyakazi ni nguzo muhimu kwa mafanikio ya muda mrefu.  Hata hivyo, changamoto ya kudhibiti wafanyakazi wasio waaminifu inaweza kuwa kubwa na yenye athari kubwa kwa biashara yako.  Wizi na udanganyifu vinaweza kusababisha hasara za kifedha, kupoteza wateja, na kuharibu sifa ya biashara.  Katika andiko hili, tutajadili njia 10 za kudhibiti wafanyakazi wasio waaminifu ili kuhakikisha biashara yako inabaki salama na yenye mafanikio. 1.KUAJIRI KWA UMAKINI Mchakato wa kuajiri ni hatua ya kwanza muhimu katika kudhibiti wafanyakazi wasio waaminifu.  Hakikisha unafanya uchunguzi wa kina wa historia ya kazi ya mwombaji, ukaguzi wa kumbukumbu za uhalifu, na mahojiano ya kina.  Uchunguzi wa historia ya kazi unajumuisha kuwasiliana na waajiri wa zamani ili kuthibitisha taarifa zilizotolewa na mwombaji.  Ukaguzi wa kumbukumbu za uhalifu unasaidia kugundua kama mwombaji ana historia ya vitendo vya uhalifu. Mahojiano ya kina yan...

AINA 5 ZA WATEJA WASUMBUFU NA NAMNA YA KUACHANA NAO

Picha
Katika biashara, wateja ni kiini cha mafanikio. Hata hivyo, si kila mteja ni mzuri kwa biashara yako. Wateja wengine wanaweza kuleta changamoto kubwa zaidi kuliko faida, na ni muhimu kujua ni wateja gani unatakiwa uachane nao ili kuboresha ufanisi na faida ya biashara yako.  Katika maelezo haya, tutachunguza aina mbalimbali za wateja ambao unaweza kuamua kuachana nao, na tutatoa mifano halisi kutoka biashara tofauti tofauti. AINA ZA WATEJA WA KUACHANA NAO 1.Wateja Wasio na Uaminifu    - Tabia: Wateja hawa wanajulikana kwa kutokuwa waaminifu katika malipo au mikataba.  Wanaweza kuchelewesha malipo au kutozingatia masharti ya mikataba.    - Mfano : Katika biashara yako unaweza kuwa na mteja ambaye kila mara anadai punguzo kubwa au anachelewesha malipo kwa muda mrefu, hivyo kuathiri mtiririko wa fedha wa biashara yako. 2.Wateja Wenye Malalamiko ya Mara kwa Mara    - Tabia : Wateja hawa wanatoa malalamiko yasiyo na msingi mara kwa mara, na wanahitaji ...

SABABU 10 ZINAZOFANYA BIASHARA NYINGI ZINAZOANZISHWA TANZANIA KUFA

Picha
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha biashara nyingi zinazoanzishwa kufa, hasa katika mazingira ya Tanzania.  Hapa kuna maelezo ya kina kuhusu baadhi ya sababu hizo na sababu ya mwisho imechangia biashara nyingi zaidi kufa. 1. Mipango Duni ya Biashara Biashara nyingi zinaanzishwa bila mipango madhubuti. Mpango wa biashara unapaswa kujumuisha malengo, mikakati ya masoko, muundo wa utawala, na makadirio ya kifedha.  Kwa mfano, mfanyabiashara anayeanzisha duka la nguo bila kujua wateja wake walengwa ni akina nani na jinsi ya kuwafikia, anaweza kushindwa kupata wateja wa kutosha. 2. Uongozi na Usimamizi Mbaya:  Uongozi bora ni muhimu kwa mafanikio ya biashara. Biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya uongozi mbovu na usimamizi duni.  Kwa mfano, kampuni inayoshindwa kusimamia vizuri rasilimali zake, kama vile wafanyakazi na fedha, inaweza kupata hasara na hatimaye kufa. 3. Kutowajali Wateja:   Wateja ni msingi wa biashara yoyote. Biashara nyingi zinakufa kwa sabab...

BIASHARA YAKO KAMA HAISIKIKI BASI HAKIKISHA INAONEKANA

Picha
Kikawaida akili ya binadamu huwa inasahau mambo kadhaa wa kadha kama endapo hayo mambo hayatumiki au hayaonekani. Mfano huwa unapoteza ujuzi ulio nao kama endapo huutumii mara kwa mara. Vilevile kuna baadhi ya vitu huwa unasahau kama huvioni mara kwa mara. Hivi ndivyo biashara yako nayo itafanikiwa kama endapo watu wataendelea kuiona au kuikumbuka mara kwa mara. Hapa tunazungumzia umuhimu wa KUITANGAZA BIASHARA YAKO siku zote. Kamwe usifanye kosa la kuacha kuitangaza biashara yako. Katika masoko kuna msemo unasema "Kama husikiki basi onekana,na kama huonekani basi sikika". Mfano nikuulize ni lini imepita hujakutana na tangazo la soda ya 'cocacola'? Cocacola ni soda ya enzi na enzi kila mtu anaijua lakini mpaka leo unaona wanaitangaza kwenye TV,redio, mtandaoni,magazetini n.k Kwa ukubwa walio nao Cocacola wangeweza acha kuingia gharama ya matangazo,lakini wanajua umuhimu wa kuendelea kuonekana au kusikika. Hata wewe hiyo bidhaa au huduma unayouza haitajulikana kama hut...

EPUKA KOSA HILI WAKATI WA KUWEKA BEI YA BIDHAA AU HUDUMA YAKO

Picha
Biashara huwa zinahitaji mikakati mbalimbali ili ziendelee kukua. Moja ya mikakati unayotakiwa kuna makini ni namna ya kuweka bei ya bidhaa au huduma yako. Kuna makosa mawili makubwa ambayo wafanyabiashara wanaweza kufanya wakati wa kuweka bei za bidhaa au huduma zao: 1. KOSA LA KWANZA-Kuuza kwa bei ndogo wakati huna mzunguko mkubwa    - Maana; Hii inamaanisha kuuza bidhaa au huduma zako kwa bei ya chini sana wakati huna wateja wengi au mzunguko mkubwa wa mauzo.    - Mfano: Fikiria una duka jipya la nguo na unauza nguo zako kwa bei ya chini sana ili kuvutia wateja.  Kwa kuwa huna wateja wengi bado, faida yako itakuwa ndogo sana na huenda usiweze kufidia gharama zako za uendeshaji.  Hii inaweza kusababisha biashara yako kufilisika haraka. 2.KOSA LA PILI-Kuuza kwa bei kubwa wakati huna jina kubwa:    - Maana : Hii inamaanisha kuweka bei za juu kwa bidhaa au huduma zako wakati huna jina kubwa au sifa nzuri sokoni.    - Mfano:  Fikiria ...

JINSI YA KUPUNGUZA GHARAMA ZA KUITANGAZA BIASHARA YAKO

Picha
Gharama za kupata wateja wapya zimekua zikiongezeka mara kwa mara. Iwe ni unatangaza biashara yako kwa njia za kawaida(traditional) au unatumia njia za kisasa za fursa za kidijitali kote gharama ni kubwa. Utatumia kwa siku kuanzia dola 4 ili kutangaza tangazo lako Instagram au Facebook ili watu wengi waone bidhaa yako. Lakini gharama za matangazo ni kubwa zaidi hasa kwenye platforms nyingine kama Tweeter(X),youtube au Google. Gharama za masoko ni kubwa hasa kwa wafanyabiashara wenye mitaji midogo. Na kumbuka SIO ukitangaza biashara yako lazima upate wateja wanaonunua,kwani kuna muda unaishia kupata watu wanaouliza bei pekee bila kununua. Hivyo ni muhimu kuwa na mikakati mingine ya ziada ya kupata wateja ukiachana na huu mkakati wa kulipia matangazo (sponsor) muda wote. Kuwa na utaratibu wa kuwaomba wateja wako wakusaidie kukuongelea mazuri kwa wengine ili waje wanunue kwako. Wafanye wateja wako sehemu ya wadau muhimu wa biashara yako ili wawe mabalozi wazuri huko nje. Inabidi ukae kich...
Picha
MAKOSA 10 UNAYOFANYA WAKATI WA KUUZA BIDHAA/HUDUMA YAKO NA NAMNA YA KUYAEPUKA Kuuza bidhaa au huduma ni sanaa ambayo lazima ufahamu kanuni zake. Ndio maana wewe na mwenzako mnaweza kuwa mnauza bidhaa au huduma inayofanana lakini mwenzio anauza zaidi ila wewe unaishia kuza kidogo. Kuna baadhi ya makosa ambayo wafanyabiashara wengi wamekua wakiyafanya mara kwa mara lakini hawajui kuwa ni makosa,na huwa yanafanya wasiuze au watumie nguvu kubwa kushawishi mteja. 1.KUTOMSIKILIZA MTEJA VIZURI Hii ni changamoto pale ambapo wewe muuzaji unakua muongeaji kupita kiasi na kutompa mteja nafasi ya kuongea au kuuliza maswali. Kimsingi wewe unatakiwa usiwe muongeaji sana zaidi ya mteja.   Fanya Hivi Tumia muda mwingi kumsikiliza vizuri mteja ana changamoto gani au anahitaji huduma ipi,na wewe jikite kumuuliza maswali machache ili ufahamu shida yake zaidi. 2.KUFOKASI KWENYE MUONEKANO WA BIDHAA BADALA YA FAIDA ILIYOPO Hii imekua changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wengi ambapo wao huzingatia zaidi...
Picha
YAFAHAMU MAMBO 5 (MATANO) ILI KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO Dunia ya biashara imekua ikibadilika mara kwa mara,hii ikiwa ni pamoja na ujuzi au mikakati mbalimbali ambayo imekua ikitumika kulingana na aina ya biashara husika nayo huwa inabadilika. Haijalishi kama ndio unaanza biashara au ni mzoefu kwenye biashara fulani itakulazimu kuendana tu na mabadiliko mbalimbali ili uweze kufanikiwa kibiashara.  Katika andiko hili tutashirikishana mambo kama matano muhimu ili kusaidia kufanya biashara yenye mafanikio ili uweze kutimiza malengo yako uliyojiwekea. 1. JENGA JINA(BUILD A BRAND) Brand ni zaidi ya nembo ya biashara yako.  Huu ni utambulisho wa biashara yako na kwa namna gani unafikisha utambulisho huo kwa wateja wako. Ukiwa na brand(jina) kubwa ni rahisi kuwa mbele ya washindani wako,na vilevile utavutia watu wengine waje kwako na pia utaongeza thamani yako sokoni.   Hivyo ni muhimu sana ukaweka mikakati ya kujenga brand yako kwa kujitofutisha na washindani wako kwa k...
Picha
  UMUHIMU WA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA BIASHARA YAKO Biashara nyingi huporomoka au nyingine hufa kabisa kutokana na kutokuwepo kwa mikakati bora ya ufuatiliaji mwenendo wa biashara husika.  Watu wengi hujikuta wamefanya matumizi makubwa mpaka wanajikuta wametumia na mtaji wa biashara. Hii husababishwa na uzembe wa kutotunza kumbukumbu au taarifa za mapato yanayoingia na matumizi. Biashara yoyote ili iweze kufanikiwa,utunzaji wa kumbukumbu ni nguzo muhimu sana. Kuna msemo huwa unasema “mali bila daftari huisha bila habari” NI KWANINI WATU HAWATUNZI KUMBUKUMBU ZA BIASHARA? Kuna sababu kadhaa ambazo huwa zinafanya watu waone shida kutunza kumbukumbu za biashara,tutaziangalia baadhi yake hapa chini. KUKOSA ELIMU YA KIBIASHARA Watu wengi huanzisha biashara kabla au pasipo kupata elimu ya kutosha kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia katika ufanyaji biashara. Na mojawapo ya elimu hizi ni pamoja na elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara.  Hivyo hujikuta wakipot...