Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya malengo

MAKOSA 10 AMBAYO WATU WENGI HUJUTIA BAADAE KATIKA MAISHA

Picha
Katika maisha, kila mtu hufanya makosa. Hata hivyo, kuna makosa fulani ambayo yanaweza kuwa na athari kubwa na ya kudumu, na mara nyingi watu hujuta baada ya kuyafanya. Makosa haya yanaweza kuathiri maisha yetu ya kibinafsi, kitaaluma, na kifedha.  Kujifunza kutoka kwa makosa ya wengine kunaweza kutusaidia kuepuka mitego hiyo na kuishi maisha yenye furaha na mafanikio zaidi. 1.Kutokuweka Akiba Watu wengi hupuuza umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya dharura na siku za usoni. Bila akiba, mtu anaweza kukumbwa na matatizo makubwa kifedha wakati wa dharura kama vile ugonjwa, kupoteza kazi, au gharama zisizotarajiwa.  Ni muhimu kuweka akiba kidogo kidogo kila mwezi ili kujenga mfuko wa dharura ambao unaweza kusaidia wakati wa matatizo.   2.Kutozingatia Afya Afya ni msingi wa maisha bora. Watu wengi hujuta kwa kutokuwekeza muda na rasilimali katika afya zao, kama vile kufanya mazoezi na kula chakula bora.  Matokeo yake ni magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu,...

FAHAMU SAIKOLOJIA YA NADHARIA YA GARI JEKUNDU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUFIKIA MALENGO YA BIASHARA AU MAISHA YAKO

Picha
Hivi umewahi jiuliza ni kwanini ukianza kukifikiria kitu fulani ni rahisi zaidi kuanza kukiona ona kila mara? Yes hii huwa inawakuta watu wengi sana. Kuna nadharia ya kiasikolojia inaitwa "Red car theory" ambayo kwa kiswahili inaitwa "Nadharia ya gari jekundu" Nadharia ya Gari Jekundu ni dhana inayohusiana na jinsi akili zetu zinavyobadilika tunapolenga kitu fulani.  Inamaanisha kwa mfano leo hii ukaanza kufikiria kuhusu gari jekundu na ukatoka nje kuanza kutazama magari mekundu,utajikuta unayona mengi. Mara nyingi, tunapoanza kufikiria kuhusu kitu fulani, tunaanza kukiona kila mahali.  Hii inaitwa "Selective Attention"au "Baader-Meinhof Phenomenon". NADHARIA YA GARI JEKUNDU INAONGELEA JUU YA  NINI HASA? 1.Umakini na Mtazamo:    Akili zetu zina uwezo mdogo wa kuchakata taarifa zote tunazopokea.  Tunapolenga kitu fulani, akili zetu zinaanza kukipa kipaumbele na kukifanya kionekane zaidi.  Kwa mfano, ukianza kufikiria kuhusu magari mekundu, utaanza...

MAENEO 6 YA KUJIFANYIA TATHIMINI BINAFSI YA MAISHA YAKO

Picha
  Kuwa na utaratibu wa kujifanyia tathimini binafsi(self-assessment) kwenye maeneo yako mbalimbali kuhusu Maisha yako. Soma maeneo yote lakini tathimini ya mwisho mwa andiko hili ni muhimu zaidi  1.KWENYE AFYA YAKO. Kuwa na utaratibu wa kujifanyia tathimini juu ya mwenendo wa afya yako. Je unafanya mazoezi ya kutosha? je unakula chakula bora? Je unaridhika na maendeleo ya afya yako sasa ukilinganisha na siku zilizopita? Je una changamoto zipi za kiafya kwa sasa ambazo unahitaji kuzifanyia kazi? n.k. 2.TATHIMINI YA KIFEDHA Ni muhimu ukawa unajifanyia tathimini binafsi kuhusu Hali yako ya kifedha kwa sasa. Je kipato chako kinatosha.? Je una utaratibu mzuri wa kibajeti na unaufuata? Je unatumia fedha yako katika maeneo gani na gani? Je huoni kuna haja ya kuongeza chanzo kingine cha mapato? Ni wapi pesa yako huwa inapotea sana? Upunguze natumizi yapi na uiwekeze wapi pesa yako kwa sasa? Je una akiba kwa ajili ya dharula n.k 3.TATHIMINI YA MAHUSIANO YAKO NA WATU Fanya tathimini juu...