Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kuuza

EPUKA KUFANYA MAKOSA HAYA 8 YATADHOOFISHA BIASHARA YAKO

Picha
Kama mfanyabiashara, unahitaji kuwa na uelewa mzuri wa jinsi ya kuendesha biashara yako kwa ufanisi.  Hii inajumuisha kuepuka makosa ambayo yanaweza kudhoofisha biashara yako.  Makosa haya yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye ukuaji na mafanikio ya biashara yako. 1.KUJIFANYA UNAJUA KILA KITU Kujifanya unajua kila kitu ni kosa kubwa. Hakuna mtu anayejua kila kitu, na kujifunza kutoka kwa wengine ni muhimu sana.  Unapojifanya unajua kila kitu, unajifunga fursa za kujifunza na kuboresha biashara yako. Mfano Mfanyabiashara mpya anaweza kufikiri kwamba anajua kila kitu kuhusu soko lake. Hata hivyo, kwa kushirikiana na wajasiriamali wazoefu na kuhudhuria semina za biashara, anaweza kujifunza mbinu mpya za kuboresha bidhaa na huduma zake. 2.KUANZA BIASHARA BILA MIUNDOMBINU Kuanza biashara bila kuwa na miundombinu ya msingi ni kosa lingine kubwa.  Miundombinu hii inajumuisha mtaji wa kutosha, vifaa muhimu, na ofisi ndogo. Bila haya, biashara yako inaweza kushindwa mapema. Mf...
Picha
MAKOSA 10 UNAYOFANYA WAKATI WA KUUZA BIDHAA/HUDUMA YAKO NA NAMNA YA KUYAEPUKA Kuuza bidhaa au huduma ni sanaa ambayo lazima ufahamu kanuni zake. Ndio maana wewe na mwenzako mnaweza kuwa mnauza bidhaa au huduma inayofanana lakini mwenzio anauza zaidi ila wewe unaishia kuza kidogo. Kuna baadhi ya makosa ambayo wafanyabiashara wengi wamekua wakiyafanya mara kwa mara lakini hawajui kuwa ni makosa,na huwa yanafanya wasiuze au watumie nguvu kubwa kushawishi mteja. 1.KUTOMSIKILIZA MTEJA VIZURI Hii ni changamoto pale ambapo wewe muuzaji unakua muongeaji kupita kiasi na kutompa mteja nafasi ya kuongea au kuuliza maswali. Kimsingi wewe unatakiwa usiwe muongeaji sana zaidi ya mteja.   Fanya Hivi Tumia muda mwingi kumsikiliza vizuri mteja ana changamoto gani au anahitaji huduma ipi,na wewe jikite kumuuliza maswali machache ili ufahamu shida yake zaidi. 2.KUFOKASI KWENYE MUONEKANO WA BIDHAA BADALA YA FAIDA ILIYOPO Hii imekua changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wengi ambapo wao huzingatia zaidi...