Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya uwekezaji

JUA FAIDA ZA KUFANYA UWEKEZAJI KWENYE HISA ZA MAKAMPUNI

Picha
Mfanyabiashara na tajiri mkubwa Duniani Warren Buffett ambaye ni muwekezaji mkubwa aliwahi kusema “ kama hutajifunza namna ya kutengenenza fedha ukiwa umelala,jua utaendelea kufanya kazi mpaka kifo chako kikukute” . Pointi ya msingi ya Warren Buffett ilikua ni msisitizo juu ya umuhimu wa kufanya uwekezaji ambao unaweza kukuingizia mapato hata bila uwepo wako(passive income). Yaani umefanya uwekezaji watu wengine au system zinaendelea kukuingizia kipato bila hata wewe kuwepo eneo husika.  Fikiria umefanya uwekezaji halafu mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka pesa inaingia tu kwenye akaunti yako bila wewe kutumia nguvu kubwa na muda. Katika andiko hili tutaelezea aina mojawapo ya uwekezaji ambao unaweza kukuingizia mapato bila uwepo wako ingawa inahitaji nguvu na jitihada kubwa mwanzoni wakati wa kuwekeza. Tutaangalia nini maana,faida,na ugumu wa kuwekeza kwenye Hisa za makampuni. Na vilevile tutaona ni mambo gani ya msingi ya kuzingatia kabla hujawekeza katika Hisa. NINI MAANA YA HISA...
Picha
 MAMBO SABA (7) YA KUZINGATIA KABLA HUJAANZISHA BIASHARA MPYA Kuanzisha biashara ni uamuzi mkubwa na mzuri ambao huwa unahitaji kujiandaa na kuwa na mpango makini.  Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla hujaanzisha biashara mpya ambayo yanaweza kufanya biashara yako ikafanikiwa au ikafa ambayo ni muhimu kuyafahamu Katika andiko hili tutangalia mambo kadhaa ya kuzingatia kabla hujafanya maamuzi hayo na ni kwa namna gani yatakusaidia ufikie malengo yako. 1. WAZO LA BIASHARA YAKO Jambo la kwanza na la muhimu la kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara mpya ni wazo la biashara unayotaka kuanzisha.  Wazo la biashara ndio msingi wa biashara yako kwani unatakiwa uwe na wazo la biashara linaloeleweka vizuri. Wazo lako la biashara ni muhimu lijibu maswali haya: Bidhaa au huduma utakayotoa ni ipi? Kwa namna gani bidhaa yako itatatua changamoto za watu au kukidhi mahitaji yao? Ni kwa namna gani huduma yako itatofautiana na ya wenzako? Wazo lako la biashara ni muhimu pia likatokana na ...
Picha
  UMUHIMU WA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA BIASHARA YAKO Biashara nyingi huporomoka au nyingine hufa kabisa kutokana na kutokuwepo kwa mikakati bora ya ufuatiliaji mwenendo wa biashara husika.  Watu wengi hujikuta wamefanya matumizi makubwa mpaka wanajikuta wametumia na mtaji wa biashara. Hii husababishwa na uzembe wa kutotunza kumbukumbu au taarifa za mapato yanayoingia na matumizi. Biashara yoyote ili iweze kufanikiwa,utunzaji wa kumbukumbu ni nguzo muhimu sana. Kuna msemo huwa unasema “mali bila daftari huisha bila habari” NI KWANINI WATU HAWATUNZI KUMBUKUMBU ZA BIASHARA? Kuna sababu kadhaa ambazo huwa zinafanya watu waone shida kutunza kumbukumbu za biashara,tutaziangalia baadhi yake hapa chini. KUKOSA ELIMU YA KIBIASHARA Watu wengi huanzisha biashara kabla au pasipo kupata elimu ya kutosha kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia katika ufanyaji biashara. Na mojawapo ya elimu hizi ni pamoja na elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara.  Hivyo hujikuta wakipot...