MAENEO 6 YA KUJIFANYIA TATHIMINI BINAFSI YA MAISHA YAKO

Kuwa na utaratibu wa kujifanyia tathimini binafsi(self-assessment) kwenye maeneo yako mbalimbali kuhusu Maisha yako. Soma maeneo yote lakini tathimini ya mwisho mwa andiko hili ni muhimu zaidi 1.KWENYE AFYA YAKO. Kuwa na utaratibu wa kujifanyia tathimini juu ya mwenendo wa afya yako. Je unafanya mazoezi ya kutosha? je unakula chakula bora? Je unaridhika na maendeleo ya afya yako sasa ukilinganisha na siku zilizopita? Je una changamoto zipi za kiafya kwa sasa ambazo unahitaji kuzifanyia kazi? n.k. 2.TATHIMINI YA KIFEDHA Ni muhimu ukawa unajifanyia tathimini binafsi kuhusu Hali yako ya kifedha kwa sasa. Je kipato chako kinatosha.? Je una utaratibu mzuri wa kibajeti na unaufuata? Je unatumia fedha yako katika maeneo gani na gani? Je huoni kuna haja ya kuongeza chanzo kingine cha mapato? Ni wapi pesa yako huwa inapotea sana? Upunguze natumizi yapi na uiwekeze wapi pesa yako kwa sasa? Je una akiba kwa ajili ya dharula n.k 3.TATHIMINI YA MAHUSIANO YAKO NA WATU Fanya tathimini juu...