
FAIDA ZA KUWA NA TOVUTI (WEBSITE) KWA AJILI YA BIASHARA AU KAMPUNI Hakuna wakati ambao website ni ya muhimu kama wakati ambapo tupo katika zama za utandawazi. Yawezekana ukajiona kuwa unachofanya ni kidogo hivyo hauhitaji website , hata hivyo kuna mengi utakua unakosa kwa kutokujikita katika kuwa na website kwa biashara au asasi yako. 1) Kukipa thamani ufanyacho Imekua kawaida watu wengi kuamini kuwa biashara au asasi yenye website basi itakua makini . Hata hivyo sio tuu website ili mradi website. Unatakiwa uwe na website ambayo kweli inaonyesha umakini na ubora wa asasi au biashara yako hii inajumuisha website yenye muonekano mzuri, yenye maelezo yaliyokamilika, yenye taarifa ambazo kweli. 2) Kuleta ushawishi Unahitaji website ili kuweza kujenga uaminifu na kuonekana kweli upo serious. Website yako itakupa nafasi ya kuwaeleza watu kwa umakini na kwa ushawishi kile unachofanya na kwanini wakutafute wewe. Tena website itakusaidia kufanya ushawishi huu kwa watu wen...