
MAKOSA 6 YATAKAYOFANYA AKAUNTI YAKO YA WASAP IFUNGWE Haya ndio makosa 6 ukiyafanya yanaweza sababisha akaunti yako ya WhatsApp izuiwe au kufungwa kabisa kutumika. 1. KUTUMIA TOLEO LISILO RASMI LA WHATSAPP Hapa ni kwa wewe unaependa kutumia App ambazo sio rasmi kwa ajili ya WhatsApp. Hapa tunamaanisha Apps kama WhatsApp GB au WhatsApp Plus,itafanya akaunti yako kufungwa. Kwani WhatsApp hawataki utumie toleo lisilo rasmi,hivyo achana na hizo WhatsApp GB na matoleo mengine ya hovyo. 2.KUTUMA VITISHO AU MAUDHUI MABAYA Kutuma ujumbe wa vitisho au kudhihaki wengine au kufanya watu wawe na hofu. Ukifanya matendo haya kwa muda mrefu utakuja kukuta akaunti yako ya WhatsApp imezuiwa kufanya kazi,hivyo kuwa makini na ujumbe wa kutishia watu. 3.UKIRIPOTIWA MARA KWA MARA NA WATU Kama endapo utakuwa unaripotiwa mara nyingi na watu basi jua muda sio mrefu akaunti yako itafungwa. Hivyo tumia WhatsApp kiustaarabu na kiusalama ili watu wasitume report kuwa unawakera. 4.KUUNGA WATU KWENYE MAGR...