Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Utapeli
Picha
 MAMBO 8 YA KUFANYA ILI USITAPELIWE MTANDAONI Matapeli mtandaoni wameongeza spidi ya kutapeli watu. Nawe inabidi ujue namna ya kuchukua tahadhari ili usitapeliwe. 1.USIFANYE MALIPO HARAKA HARAKA Hata kama umeona bidhaa au huduma inakuvutia kwa mara ya kwanza hasa kwa mtu usiemfahamu usikimbilie kulipia haraka  Jipe muda huenda ni hisia zako za tamaa zinakufosi ulipie kwa sasa. Kumbuka matapeli wana lugha ya kuvutia sana. 2.KUWA MAKINI NA VITU AU HUDUMA ZA BEI NDOGO SANA Kuna wale watu wanatangaza wanauza vitu au huduma kwa BEI ndogo sana. Hadi unajiuliza anapataje faida? Kuwa makini matapeli huwa wanaweka vitu bei ndogo ili kukuvutia ili ukilipia tu basi humpati tena. 3.FANYA UTAFITI KUHUSU TAARIFA ZA MHUSIKA Kabla hujalipia bidhaa au huduma kwa mtu usiemfahamu ni vizuri kufanya utafiti kwanza. Angalia mawasiliano yake,anapatikana wapi, na vitu vingine vingi. Mara nyingi matapeli taarifa zao huwa zimejificha ficha hazieleweki,ukijaribu kumpigia simu au video call hapokei au h...