Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya taasisizafedha
Picha
 MAMBO MATANO (5) YA KUZINGATIA KABLA YA KUCHUKUA MKOPO WA BIASHARA BENKI Kabla ya kuchukua mkopo wa biashara toka taasisi ya fedha au taasisi binafsi ni muhimu ukafanya uchambuzi yakinifu juu ya mkopo husika. Kumbuka mikopo huwa inatolewa kwa masharti kadhaa ikiwemo kuuzwa kwa dhamana ulizoweka kwa ajili ya kulinda mkopo husika.  Hivyo elewa kabisa kama umechukua mkopo bila kuelewa misingi ya namna bora ya matumizi ya mkopo inaweza ikakuletea changamoto baadae. 1.KUWA NA LENGO LA MKOPO Ni muhimu kuwa na kuelewa hasa unahitaji mkopo kwa ajili ya lengo lipi,au unachukua tu mkopo kwasababu umesikia kuna sehemu wanatoa mikopo kiwepesi nawe unaenda kuchukua. Je lengo la kuchukua mkopo ni kwa ajili ya kuwekeza kwenye nini kwenye hiyo biashara yako.  Epuka kuchukua mkopo wa biashara lakini unachepusha kupeleka kwenye matumizi mengine nje ya lengo la mkopo Weka pesa ya mkopo kwenye biashara kama lengo husika ulivyopanga alafu matumizi yako binafsi yatoke kwenye faida utakayopata...