Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya mtaji
Picha
FAHAMU BIASHARA 19 ZA KUANZA NA MTAJI MDOGO ZENYE FAIDA Tuangalie biashara 19 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000(laki moja) unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa. Hakuna biashara ndogo, ila kuna biashara unazoweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa. Hiyo ambayo inaitwa “biashara ndogo” ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku itakutoa. Kabla hatujaenda kwenye hiyo orodha ya hizo biashara za mtaji mdogo, hebu tuweke sawa kauli ya “zenye faida kubwa”. Faida kubwa haimaanishi mamilioni ya fedha, bali ni kwamba faida utakayoipata kulingana na mtaji wako ni nzuri na usipokata tamaa itakufikisha mbali. ZINGATIA: Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile, ni vyema kufuatilia utaratibu na sheria za mahali ulipo. Tafadhali ilinde biashara yako kwa kufuata kanuni zote zilizowekwa na serikali. Baada ya kulisawazisha hilo, twende kwenye hiyo orodha ya biashara za mtaji md...
Picha
YAFAHAMU MAMBO 5 (MATANO) ILI KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO Dunia ya biashara imekua ikibadilika mara kwa mara,hii ikiwa ni pamoja na ujuzi au mikakati mbalimbali ambayo imekua ikitumika kulingana na aina ya biashara husika nayo huwa inabadilika. Haijalishi kama ndio unaanza biashara au ni mzoefu kwenye biashara fulani itakulazimu kuendana tu na mabadiliko mbalimbali ili uweze kufanikiwa kibiashara.  Katika andiko hili tutashirikishana mambo kama matano muhimu ili kusaidia kufanya biashara yenye mafanikio ili uweze kutimiza malengo yako uliyojiwekea. 1. JENGA JINA(BUILD A BRAND) Brand ni zaidi ya nembo ya biashara yako.  Huu ni utambulisho wa biashara yako na kwa namna gani unafikisha utambulisho huo kwa wateja wako. Ukiwa na brand(jina) kubwa ni rahisi kuwa mbele ya washindani wako,na vilevile utavutia watu wengine waje kwako na pia utaongeza thamani yako sokoni.   Hivyo ni muhimu sana ukaweka mikakati ya kujenga brand yako kwa kujitofutisha na washindani wako kwa k...