Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya hisa

MAMBO YA KUZINGATIA NA KUTOFANYA WAKATI WA KUANZISHA KAMPUNI YAKO

Picha
Kuanzisha kampuni ni hatua muhimu na yenye changamoto nyingi. Ni muhimu kuzingatia mambo mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kampuni yako inafanikiwa na kuepuka makosa yanayoweza kuathiri biashara yako.  Hapa kuna mambo ya kuzingatia na mambo ya kutofanya wakati wa kuanzisha kampuni nchini Tanzania. MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANZISHA KAMPUNI 1.Chagua Wazo Bora la Biashara:  Hakikisha unachagua wazo la biashara ambalo unalimudu vyema na linaweza kutekelezeka. Epuka kuchagua wazo pana sana au kwa sababu mwingine analifanya. 2.Fanya Utafiti wa Biashara:  Kabla ya kuanzisha kampuni, fanya utafiti wa kina juu ya biashara utakayofanya.  Elewa biashara yako, huduma utakayotoa, wateja wako, ushindani, na watu utakaofanya nao kazi. Mfano : Kabla ya kuanzisha kampuni ya usafirishaji, fanya utafiti wa soko ili kuelewa mahitaji ya wateja, ushindani uliopo, na gharama za kuendesha biashara.  Unaweza kuzungumza na wamiliki wa biashara za usafirishaji, kufanya tafiti za mtand...

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA

Picha
Kampuni ni chombo muhimu katika ulimwengu wa biashara, kinachowezesha watu kuunganisha rasilimali zao na kufanya shughuli za kiuchumi kwa pamoja.  Kampuni inaweza kuwa na umiliki wa watu binafsi, familia, au hata wawekezaji wengi. Katika muktadha wa Tanzania, kampuni ni njia bora ya kuendesha biashara kwa ufanisi na kupata faida kubwa. MAANA YA KAMPUNI  Kampuni ni asasi au shirika linalotambulika kisheria ambalo limeundwa kwa ajili ya kuunda au kuuza bidhaa na/au huduma kwa wateja.  Kampuni ina sifa ya kuwa na utu wa kisheria tofauti na wamiliki wake, kumiliki mali zake, na kuwa na uwezo wa kushtaki na kushtakiwa kwa jina lake. Faida za Kuwa na Kampuni 1.Utu wa Kisheria:  Kampuni inatambulika kisheria kama mtu binafsi, tofauti na wamiliki wake. Hii inamaanisha kuwa kampuni inaweza kumiliki mali, kuwa na madeni, na kuingia mikataba kwa jina lake. 2.Uwezo wa Kukusanya Mtaji:   Kampuni inaweza kukusanya mtaji kwa kuuza hisa kwa wawekezaji. Hii inasaidia kampuni kup...

JUA FAIDA ZA KUFANYA UWEKEZAJI KWENYE HISA ZA MAKAMPUNI

Picha
Mfanyabiashara na tajiri mkubwa Duniani Warren Buffett ambaye ni muwekezaji mkubwa aliwahi kusema “ kama hutajifunza namna ya kutengenenza fedha ukiwa umelala,jua utaendelea kufanya kazi mpaka kifo chako kikukute” . Pointi ya msingi ya Warren Buffett ilikua ni msisitizo juu ya umuhimu wa kufanya uwekezaji ambao unaweza kukuingizia mapato hata bila uwepo wako(passive income). Yaani umefanya uwekezaji watu wengine au system zinaendelea kukuingizia kipato bila hata wewe kuwepo eneo husika.  Fikiria umefanya uwekezaji halafu mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka pesa inaingia tu kwenye akaunti yako bila wewe kutumia nguvu kubwa na muda. Katika andiko hili tutaelezea aina mojawapo ya uwekezaji ambao unaweza kukuingizia mapato bila uwepo wako ingawa inahitaji nguvu na jitihada kubwa mwanzoni wakati wa kuwekeza. Tutaangalia nini maana,faida,na ugumu wa kuwekeza kwenye Hisa za makampuni. Na vilevile tutaona ni mambo gani ya msingi ya kuzingatia kabla hujawekeza katika Hisa. NINI MAANA YA HISA...