MAMBO 8 YA KUFANYA ILI USITAPELIWE MTANDAONI
Matapeli mtandaoni wameongeza spidi ya kutapeli watu.
Nawe inabidi ujue namna ya kuchukua tahadhari ili usitapeliwe.
1.USIFANYE MALIPO HARAKA HARAKA
Hata kama umeona bidhaa au huduma inakuvutia kwa mara ya kwanza hasa kwa mtu usiemfahamu usikimbilie kulipia haraka
Jipe muda huenda ni hisia zako za tamaa zinakufosi ulipie kwa sasa.
Kumbuka matapeli wana lugha ya kuvutia sana.
2.KUWA MAKINI NA VITU AU HUDUMA ZA BEI NDOGO SANA
Kuna wale watu wanatangaza wanauza vitu au huduma kwa BEI ndogo sana.
Hadi unajiuliza anapataje faida?
Kuwa makini matapeli huwa wanaweka vitu bei ndogo ili kukuvutia ili ukilipia tu basi humpati tena.
3.FANYA UTAFITI KUHUSU TAARIFA ZA MHUSIKA
Kabla hujalipia bidhaa au huduma kwa mtu usiemfahamu ni vizuri kufanya utafiti kwanza.
Angalia mawasiliano yake,anapatikana wapi, na vitu vingine vingi.
Mara nyingi matapeli taarifa zao huwa zimejificha ficha hazieleweki,ukijaribu kumpigia simu au video call hapokei au hapatikani.
4.CHUNGUZA VIZURI AKAUNTI ZAKE ZA MTANDAONI
Chunguza vizuri akaunti za mhusika mtandaoni zina muda gani.
Kuwa makini na akaunti mpya na zenye posti chache mara nyingi matapeli huwa wanafungua akaunti mpya kila mara.
Angalia shuhuda mbalimbali za wateja aliowauzia huko nyuma.
Angalia kama akaunti husika imekamilika kuanzia kwenye BIO na namba za simu.
Cheki link anazotumia zinakupeleka kwenye page gani na hizo page zinahusu nini.
Matapeli taarifa zao huwa hazipo kamili yaani zinajichanya.
5.IKIWEZEKANA NENDA DUKANI AU OFISINI KWAKE
Kama unaona huelewi elewi muombe uende ukaone ofisi yake au duka au muonane kabisa.
Hii itakusaidia kuondoa hofu yako na pia kupunguza kutapeliwa hasa kwa bidhaa au huduma zinazohitaji malipo makubwa
6.KAMA NI MKOPO EPUKA KULIPIA PESA YA AWALI
Kuna wale wanatoa mikopo online au wanauza vitu kwa mkopo.
Kuwa makini wengine huwa wanasema tuma pesa ya kianzio kama ya fomu ya mkopo,au akiba hapo ndio njia kuu ya matapeli.
Pindi ukituma tu pesa ya awali na tapeli atakublock hutamuona tena.
7.SIKILIZA HISIA ZA MOYO WAKO.
Kuna kitu unaweza kukipenda na ukaona sio matapeli lakini moyo wako unagoma au kusita kufanya malipo.
Usiupuuze usikilize moyo wako acha kwanza kulipia jipe muda huenda baadae ukapata wazo jingine na ukaepuka kutapeliwa.
8.ULIZA WATU KUHUSU HICHO KITU/HUDUMA
Usipende kujiingiza kwenye kufanya malipo kama mtu humjui mtandaoni.
Ulizia wengine,kama ni ndugu au marafiki,kuwa "Rafiki yangu nataka ninunue kitu fulani mtandaoni" msikie nae anakwambia nini.
Usiri umefanya wengi wapoteze pesa mtandaoni.
IMEANDIKWA NA
Mchumi Digital
0714260266
#mtandaoni #utapeli
MFANYABIASHARA JIUNGE BURE NA GROUP LETU LA WASAP ILI KUPATA HUDUMA NA MASOMO YETU MUDA WAOTE👇👇


Maoni
Chapisha Maoni