MAKOSA 10 UNAYOFANYA WAKATI WA KUUZA BIDHAA/HUDUMA YAKO NA NAMNA YA KUYAEPUKA
Kuuza bidhaa au huduma ni sanaa ambayo lazima ufahamu kanuni zake. Ndio maana wewe na mwenzako mnaweza kuwa mnauza bidhaa au huduma inayofanana lakini mwenzio anauza zaidi ila wewe unaishia kuza kidogo.
Kuna baadhi ya makosa ambayo wafanyabiashara wengi wamekua wakiyafanya mara kwa mara lakini hawajui kuwa ni makosa,na huwa yanafanya wasiuze au watumie nguvu kubwa kushawishi mteja.
1.KUTOMSIKILIZA MTEJA VIZURI
Hii ni changamoto pale ambapo wewe muuzaji unakua muongeaji kupita kiasi na kutompa mteja nafasi ya kuongea au kuuliza maswali.
Hii ni changamoto pale ambapo wewe muuzaji unakua muongeaji kupita kiasi na kutompa mteja nafasi ya kuongea au kuuliza maswali.
Kimsingi wewe unatakiwa usiwe muongeaji sana zaidi ya mteja.
Fanya Hivi
Tumia muda mwingi kumsikiliza vizuri mteja ana changamoto gani au anahitaji huduma ipi,na wewe jikite kumuuliza maswali machache ili ufahamu shida yake zaidi.
2.KUFOKASI KWENYE MUONEKANO WA BIDHAA BADALA YA FAIDA ILIYOPO
Hii imekua changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wengi ambapo wao huzingatia zaidi muonekano wa bidhaa au huduma zao badala ya kujikita kumuelekeza mteja FAIDA zinazopatikana kwenye bidhaa au huduma husika.
Kumbuka mteja huwa anataka apate faida inayopatikana na sio vitu vingine.
Fanya hivi
Tafsiri faida inayopatikana kwenye muonekano wa bidhaa yako.
Usiseme 'Kiatu hiki ni kizuri nunua" ila sema "kiatu hiki ni imara kitakupunguzia gharama ya kununua kiatu kingine ndani ya muda mfupi"
3.KUTOA AHADI ZA UONGO KUHUSU BIDHAA/HUDUMA
Kusema ahadi ambazo sio za kweli kuhusu bidhaa au huduma yako wakati unajua kabisa huwezi kuzitimiza au bidhaa yako haina hicho kitu unachokisema.
Mteja anakua na matarajio makubwa toka kwenye bidhaa au huduma lakini sio kweli.
Fanya hivi
Kuwa mkweli na muwazi usipende kumpa matumaini makubwa mteja ambayo si ya kweli.
Ni bora uweke ahadi ndogo lakini mteja aende akakutane na matokeo makubwa ya huduma au bidhaa yako.
4.KUTOKUBALI MAPINGAMIZI YA MTEJA
Kupenda kumbishia mteja juu ya jambo fulani analoliamini kuhusu bidhaa au huduma yako ni kosa ambalo wengi tunalifanya.Ndio kuna wateja wanakera lakini inatakiwa uwasikilize mapingamizi yao.
Fanya Hivi
Kwakua wewe ni mfanyabiashara basi usiogope mapingamizi au maswali toka kwa mteja.
Sikiliza vizuri usibishe na tolea ufafanuzi kiundani ili kumridhisha mteja wako.
5.KUTOWAFUATILIA WATEJA MARA NYINGINE(FOLLOWUP)
Unaweza kukutana na mteja ambae amekuahidi kuwa atakua tayari kununua bidhaa yako baada ya siku kadhaa kutokana na sababu mbalimbali.
Sasa kitendo cha kutochukua mawasiliano ya mteja ili kuwasiliana nae hiyo siku husika imekua ni kosa linalofanywa na wafanyabiashara wengi.
Na mwisho wa siku mteja hafuatiliwi ili kukumbushwa na hatimae anapotea.
Fanya hivi
Weka utaratibu wa kuweka kumbukumbu ili kuwafuatilia wale wateja ambao wametoa ahadi ya kununua siku nyingine hiyo bidhaa au huduma yako.
6.KULAZIMISHA SANA KUUZA HAPO HAPO
Kuna nyakati unajikuta unafosi mteja anaunue hapo hapo siku ya kwanza. Hii humfanya mteja awe na wasiwasi juu ya huduma au bidhaa yako.
Kuuza ni uvumilivu,kwani kuna baadhi ya bidhaa au huduma inatakiwa ujenge mahusiano na mteja kwanza ili afanye maamuzi ya kununua
Fanya hivi
Jenga mahusiano na mteja kwanza kwa kueleza faida na thamani ya bidhaa au huduma yako na mpe muda mteja afanye maamuzi ya kununa kwa spidi yake,kwani kuna ,mazingira sio lazima kufosi mauzo hapo hapo.
7.KUPOTEZA MUDA KWA MTU ASIE MTEJA
Lazima uwe na ujuzi wa kumtambua haraka mtu ambae sio mteja na hawezi kununua hiyo bidhaa yako.
Vinginevyo utajikuta unatumia nguvu kubwa na muda mwingi kwa mtu ambae hana uwezo wa kununua.
Fanya hivi
Lazima umuulize mteja maswali mengi ili kujua kama anaweza kununua,je, anayo bajeti?,ana uhitaji kwa sasa?,je ana changamoto?
Hii itasaidia kuweka nguvu kubwa kwa wale wateja ambao wana uwezekano mkubwa wa kununua bidhaa au huduma yako.
8.KUMPUUZA MSHINDANI WAKO
Kutozingatia bidhaa anayouza mpinzani yako inayofanana na yako na jinsi gani ya kujitofautisha nae.
Hii huwa inafanya ushindwe kujua namna gani wewe utafanya ili uweze kudaka wateja wako kiurahisi tofauti na mpinzani wako.
Fanya hivi
Zingatia mpinzani wako anauzaje bidhaa au huduma kama yako,ili wewe ujue namna gani ya kuithaminisha bidhaa au huduma yako ili kujua namna ya kuwashawishi wateja wako.
Usichukulie kawaida washindani wako.
9.KUTOTUMIA SHUHUDA ZA WATEJA WALIO WAHI KUNUNUA KWAKO
Hili ni kosa pale ambapo unashindwa kuwa na shuhuda za wateja wako ambao umewahi fanya nao kazi,au umewahi wauzia hiyo bidhaa au huduma yako.
Kumbuka ni ngumu sana kumshawishi mteja mpya kununua kwako kama hakujui.
Fanya hivi
Waonyeshe wateja wako shuhuda za wateja wako ambao walifanikiwa baada ya kununua bidhaa au kutumia hiyo huduma yako.
Hii itakurahisishia kuaminika kwa haraka,maana wateja wanapenda kununua baada ya kuona kuna watu wengine wamefanikiwa baada ya kutumia huduma au bidhaa fulani.
10.KUTOA MAELEZO MENGI KWA MTEJA YASIYO HITAJIKA
Kumjazia mteja kila aina ya taarifa sio ndio kwamba utauza. Na sio kila mteja utamshawishi kwa kutumia mbinu zilezile ulizokalili.
Kuna wateja huwa wanahitaji uelezee kiufupi bidhaa au huduma yako basi.
Mteja huwa hapendi kuchoshwa na taarifa nyingi ambazo hata hazina maana sana kwake.
Fanya Hivi
Msome mteja ana changamoto gani,muulize maswali ili uweze kujua maelezo gani yatamfaa ili kumshawishi,acha kukariri na kutoa kila taarifa ya huduma au bidhaa yako,maana nyingine hazina umuhimu wowote.
IMEANDIKWA NA
Mchumi Consulting
0714260266
MFANYABIASHARA JIUNGE BURE NA GROUP LETU LA WASAP ILI KUPATA HUDUMA NA MASOMO YETU MUDA WOTE HAPO CHINI👇👇
Maoni
Chapisha Maoni