MAENEO 6 YA KUJIFANYIA TATHIMINI BINAFSI YA MAISHA YAKO

 

Kuwa na utaratibu wa kujifanyia tathimini binafsi(self-assessment) kwenye maeneo yako mbalimbali kuhusu Maisha yako.
Soma maeneo yote lakini tathimini ya mwisho mwa andiko hili ni muhimu zaidi 

1.KWENYE AFYA YAKO.
Kuwa na utaratibu wa kujifanyia tathimini juu ya mwenendo wa afya yako.
Je unafanya mazoezi ya kutosha?
je unakula chakula bora?
Je unaridhika na maendeleo ya afya yako sasa ukilinganisha na siku zilizopita?
Je una changamoto zipi za kiafya kwa sasa ambazo unahitaji kuzifanyia kazi? n.k.

2.TATHIMINI YA KIFEDHA
Ni muhimu ukawa unajifanyia tathimini binafsi kuhusu Hali yako ya kifedha kwa sasa.
Je kipato chako kinatosha.?
Je una utaratibu mzuri wa kibajeti na unaufuata?
Je unatumia fedha yako katika maeneo gani na gani?
Je huoni kuna haja ya kuongeza chanzo kingine cha mapato?
Ni wapi pesa yako huwa inapotea sana?
Upunguze natumizi yapi na uiwekeze wapi pesa yako kwa sasa?
Je una akiba kwa ajili ya dharula n.k

3.TATHIMINI YA MAHUSIANO YAKO NA WATU
Fanya tathimini juu ya ubora wa mahusiano yako na familia,ndugu na marafiki zako
 
Je una mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka?
Je una mawasiliano mazuri na marafiki,ndugu na familia?
Je kazini kwako au kwenye biashara yako una migogoro?
Je wewe ni msaada kwa wenzako au umekua mzigo kwao?
Je wewe ni mtu wa kutegemewa kwenye shida na raha au upo upo tu?
Je unatumia muda wako kuwa na familia yako? N.k

4.TATHIMINI KUHUSU KAZI/BIASHARA YAKO 
Inabidi ufanye tathimini kwenye eneo la kazi yako au biashara yako maendeleo yake.
Je unaifurahia kazi hiyo unayoifanya kwa sasa?
Je pafomansi yako inaridhisha?
Je biashara yako inapanda au inashuka?
Kuna haja ya kubadilisha mbinu ili kunasa wateja wapya wa biashara yangu?
Kuna haja ya kuongeza elimu au maarifa zaidi ili niwe bora zaidi?
Je nimefikia malengo yangu kikazi kwa kiasi gani mpaka sasa?
Je Nina mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzangu au wafanyabiashara wenzangu? N.k

5.TATHIMINI YA KIROHO
Hapa unajifanyia tathimini binafsi ya kiroho.
Kwasababu unaamini kuwa hukujileta mwenyewe hapa Duniani.
Lazima ujipe muda kujifanyia tathimini juu ya mahusiano yako na Muumba wako.
Je unatenga muda kumshukuru?
Je unatoa sadaka?
Je unasali?
Hii itakusaidia zaidi kuweza kufanya maboresho zaidi katika eneo hilo.

6.TATHIMINI JUU YA MATUMIZI YA MUDA.
Ni muhimu ukajifanyia tathimini binafsi juu ya matumizi yako binafsi ya muda.
Muda ndio rasilimali ambayo ikipotea hairudi tena.
Je unatumia muda vizuri?
Je unatumia muda katika mambo yanayokuletea thamani?
Je unabalansi muda kati ya kazi na familia?
Je wewe ni mtu wa kuahirisha mambo mara kwa mara na kipi ufanye?
Je huwa unatimiza malengo yako ndani ya muda uliowekwa? N.K
Ukiwa na utaratibu wa kujifanyia tathimini binafsi kwenye angalau mambo hayo hapo juu itakua rahisi kuweza kufanikiwa kiurahisi kwenye malengo yako mbalimbali.

IMEANDIKWA NA
Mchumi Consulting 
0714260266

MFANYABIASHARA JIUNGE NA GROUP LETU LA WASAP ILI KUPATA MASOMO NA UPDATES ZA HUDUMA ZETU MUDA WOTE
👇🏻👇🏻👇🏻

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA