ZINGATIA HATUA HIZI 6 ILI UFIKIE UHURU WAKO WA KIFEDHA KIURAHISI
Kila mmoja huwa ana ndoto fulani ya kuwa siku moja awe na pesa nyingi ili aweze kutimiza mahitaji mbalimbali.
Lakini huwezi kufikia uhuru huo wa kifedha kama endapo hutachukua hatua kadhaa sasa.
Tumeelezea baadhi ya hatua sita(6) ambazo ukizichukua zitakufanya uepukane na suala la kuhangaika na uhaba wa kifedha mara kwa mara.
1. FUTA MADENI YENYE RIBA KUBWA
Moja ya kitu kinachomaliza pesa zako ni madeni yenye riba kubwa.
Ni kweli mkopo sio mbaya lakini pale ambapo unachukua mikopo yenye riba kubwa sana huwa inaumiza.
Kumbuka riba ni gharama ya mkopo uliochukua,lakini kama endapo utakua na mikopo mingi yenye riba kubwa jua kiasi kikubwa cha pesa utakua unatumia kulipa riba za mikopo, na kuwafaidisha waliokupa mkopo,hivyo kuwa makini kwenye hili.
2.PUNGUZA MATUMIZI YASIYO NA ULAZIMA
Anza sasa kujifanyia tathimini juu ya matumizi yako kwenye vitu unavyopenda kununua.
Jilulize je hiki kitu kina umuhimu kwa sasa,au niachane nacho ili hii pesa itumike kwenye jambo la muhimu zaidi ya hili.
Unaweza kuwa na mapato mengi ya fedha lakini kama una matumizi yasiyo na ulazima itakuwia ugumu kufikia uhuru wa kifedha kiurahisi
3.ISHI MAISHA YA KIPATO CHAKO
Anza sasa kuishi maisha yanayolingana na kipato chako.
Acha kasumba ya kuiga au kushindana na watu waliokuzidi Maisha.
Wengi hawafiki uhuru wa kifedha kwasababu ya kutumia pesa kwa kuishi maisha yaliyo juu ya mapato yao.
4.WEKA AKIBA NA WEKEZA
Ni muhimu pesa unayopata ukaiwekeza maeneo tofauti tofauti kama kwenye biashara n.k
Lakini vilevile kuwa na utaratibu wa kuweka akiba maana itakusaidia kwenye matukio ya dharula lakini akiba inaweza kutumika baadae kwa ajili ya uwekezaji fulani.
Hii itakusaidia kurahisisha mbio zako za kuelekea uhuru wa kifedha kiurahisi.
5.ACHA MAISHA YA KUIGA WENGINE
Hapa Duniani kila mtu ana njia zake za kuingiza kipato.
Hivyo kama utatumia muda wako mwingi kujifananisha na wengine utajikuta wewe unaishiwa ila wenzio hawaishiwi pesa.
Usipende kuiga kufanya matumizi kama wengine wakati unajijua kipato chako ni kidogo kuliko wenzako.
Anza sasa kuishi maisha yako yenye malengo yako ya kufikia uhuru wa kifedha.
6.TAFUTA KIPATO CHA ZIADA
Ni muda muafaka sasa ukaanza kufikiria kuanzisha chanzo kingine cha mapato ili kisaidiane na chanzo chako ulicho nacho sasa.
Kumbuka shuhuda za watu wengi waliofanikiwa kipesa huwa hawana chanzo kimoja cha mapato.
Hii husaidia kuweza kufikia malengo yako kifedha kiurahisi.
IMEANDIKWA NA
Mchumi Consulting
0714260266
Maoni
Chapisha Maoni