MAKOSA 6 YATAKAYOFANYA AKAUNTI YAKO YA WASAP IFUNGWE
Haya ndio makosa 6 ukiyafanya yanaweza sababisha akaunti yako ya WhatsApp izuiwe au kufungwa kabisa kutumika.
1. KUTUMIA TOLEO LISILO RASMI LA WHATSAPP
Hapa ni kwa wewe unaependa kutumia App ambazo sio rasmi kwa ajili ya WhatsApp.
Hapa tunamaanisha Apps kama WhatsApp GB au WhatsApp Plus,itafanya akaunti yako kufungwa.
Kwani WhatsApp hawataki utumie toleo lisilo rasmi,hivyo achana na hizo WhatsApp GB na matoleo mengine ya hovyo.
2.KUTUMA VITISHO AU MAUDHUI MABAYA
Kutuma ujumbe wa vitisho au kudhihaki wengine au kufanya watu wawe na hofu.
Ukifanya matendo haya kwa muda mrefu utakuja kukuta akaunti yako ya WhatsApp imezuiwa kufanya kazi,hivyo kuwa makini na ujumbe wa kutishia watu.
3.UKIRIPOTIWA MARA KWA MARA NA WATU
Kama endapo utakuwa unaripotiwa mara nyingi na watu basi jua muda sio mrefu akaunti yako itafungwa.
Hivyo tumia WhatsApp kiustaarabu na kiusalama ili watu wasitume report kuwa unawakera.
4.KUUNGA WATU KWENYE MAGROUP BILA RUHUSA YAO
Acha tabia ya kuunga watu kwenye magrop ya WhatsApp bila ruhusa yao.
WhatsApp wanataka upate ruhusa ya mtu kabla hujamuunga kwenye group lolote la WhatsApp.
Watumie watu link ili wajiunge kwa hiari sio kufosi kuwaunga kwenye group lako.
Na hata ikitokea wamekuruhusu kuwaunga basi waunge polepole au kidogo kidogo,sio unataka shortcut za kuunga watu 300 ndani ya dakika moja,jua hapo WhatsApp watajua wewe ni roboti na akaunti yako itafungwa
5. KUSAMBAZA HABARI ZA UONGO NA LINK ZA UTAPELI
Acha tabia ya kusambaza taarifa za uwongo,au umbea ambao unajua sio wa kweli.
Au kusambaza link za kitapeli kwa watu.
Kusambaza ujumbe wa aina hiyo ni kwenda kinyume na sera ya WhatsApp,wataizuia akaunti yako au wataifunga moja kwa moja.
6.KUTUMIA APP ZA AUTOMATIKI KUTUMA AU KUJIBU MESEJI
Kuna wale wanapenda kuweka automations za kujibu meseji au kutuma mameseji mengi kwa mara moja.
Wengine hutumia mfumo wa kutumia 'Bots' kujibu meseji au kutuma message.
Unaweza ukafanya hivyo akaunti isifungwe,lakini baada ya muda system za WhatsApp zikikusoma basi jua WhatsApp yako itazuiwa.
WhatsApp wanapenda binadamu husika ndio atume au ajibu meseji na sio kutumia robot ndio lifanye kazi yako.
MWISHO epuka akaunti yako kuzuiwa au kufungwa kabisa kwa kufuata sheria na sera za WhatsApp na penda kuheshimu watumiaji wengine.
Imeandikwa na
Mchumi Consulting
0714 260266
MFANYABIASHARA JIUNGE BURE NA GROUP LETU LA WASAP ILI KUPATA HUDUMA NA MASOMO YETU MUDA WOTE👇👇
Maoni
Chapisha Maoni