MAMBO MATANO (5) YA KUZINGATIA KABLA YA KUCHUKUA MKOPO WA BIASHARA BENKI
Kabla ya kuchukua mkopo wa biashara toka taasisi ya fedha au taasisi binafsi ni muhimu ukafanya uchambuzi yakinifu juu ya mkopo husika.
Kumbuka mikopo huwa inatolewa kwa masharti kadhaa ikiwemo kuuzwa kwa dhamana ulizoweka kwa ajili ya kulinda mkopo husika.
Hivyo elewa kabisa kama umechukua mkopo bila kuelewa misingi ya namna bora ya matumizi ya mkopo inaweza ikakuletea changamoto baadae.
1.KUWA NA LENGO LA MKOPO
Ni muhimu kuwa na kuelewa hasa unahitaji mkopo kwa ajili ya lengo lipi,au unachukua tu mkopo kwasababu umesikia kuna sehemu wanatoa mikopo kiwepesi nawe unaenda kuchukua.
Je lengo la kuchukua mkopo ni kwa ajili ya kuwekeza kwenye nini kwenye hiyo biashara yako.
Epuka kuchukua mkopo wa biashara lakini unachepusha kupeleka kwenye matumizi mengine nje ya lengo la mkopo
Weka pesa ya mkopo kwenye biashara kama lengo husika ulivyopanga alafu matumizi yako binafsi yatoke kwenye faida utakayopata baada ya pesa ya mkopo kuingia kwenye biashara yako. Hili ni eneo la msingi sana kuzingatia.
2.FAHAMU UWEZO WA BIASHARA YAKO
Hili ni eneo linalohitaji mazingatio makubwa sana kwa mfanyabiashra maana ni muhimu kujua uwezo wakifedha wa biashara yako.
Na ni muhimu kujua uwezo wa biashara yako wa kutoa faida ndani ya muda fulani. Hii itasaidia kuweza kuchukua kiwango kile cha mkopo ambacho biashara yako ina uwezo wa kumudu.
Mfano unajua kabisa kwa mwezi biashara yako ina uwezo wa kuingiza faida ya milioni moja,lakini wewe unakwenda kuchukua mkopo wenye rejesho la milioni tatu kwa mwezi ambalo ni maratatu zaidi ya faida unayoingiza.
Kufanya hivyo kutafanya mkopo na matumizi mengine yaielemee biashara yako na utaanza kupata shida namna ya kurejesha mkopo kwa wakati au utarejesha kwa changamoto nyingi.
3. ANDAA MPANGO WA BIASHARA YAKO
Ni muhimu kabla hujachukua mkopo kuwa na mipango uliyoiandaa kabisa kuhusu biashara yako.
Mipango inaweza kuwa ya muda mfupi, kati au ya muda mrefu na vilevile uandae mikakati ya kuifikia hiyo mipango ya biashara yako.
Sio unachkua mkopo ndio unaanza kuweka mipango ya wapi kiende hiki na wapi pesa fulani iende.
Kumbuka ukichukua mkopo hapohapo riba zinaanza kusoma na muda si mrefu utahitajika uanze kulipa marejesho ya mkopo husika.
sasa kama ulikua huna miapango hapo kabla basi jua mkopo Unaweza ukakusumbua namna ya ulipaji.
4. KUWA NA TAARIFA SAHIHI ZA KIFEDHA
Ni wajibu wako kama mfanyabiashara ukawa na taarifa sahihi za kifedha kuhusu biashara yako.
Taarifa za kifedha ni kama vile mapato unayoingiza pamoja na gharama unazoingia ndani ya muda fulani.
Ni muhimu kujua rekodi hizi muhimu ili ujue kiwango cha mkopo unachopaswa kuchukua ndani ya muda fulani.
Usipokua na taarifa hizi itafanya uchukue mkopo mkubwa sana au unaweza chukua mkopo mdogo ambao kimsingi unaweza usitimize malengo ya uwekezaji kwenye biashara yako
Na kama endapo utakua hujui hesabu zako,unaweza chukua mkopo na ukashiundwa kutengenenza faida kwenye biashara yako,na mwisho wa siku mkopo unaweza kukushinda
5. JUA KUHUSU RIBA NA MASHARTI YA MKOPO
Jambo linguine la msingi la kuzingatia kabala hujafanya maamuzi ya kuchukua mkopo ni kuzingatia rib na masharti ya mkopo husika.
Fanya utafiti ni benki au taasisi gani ina rib ana masharti nafuu kwa mkopeshaji.
Ukiachana na riba pata na elewa taarifa zaidi juu ya gharama za ziada za mkopo husika.
Gharama za ziada za mkopo zinaweza kuwa ni ada ya mkopo,bima ya mkopo,gharama za mwanasheria na nyinginezo.
Masharti ya mkopo yanaweza kuwa ni dhamana unazotakiwa kuwa nazo,namna ya ulipaji wa mkopo wako,kama utalipa kwa muda gani na mwenendo wa ulipaji(payment schedule)
Elewa vizuri aina ya riba unayopewa,kama ni ile inayobadilika badilika kulingana na kiwango cha mkopo kilichobakia(decline interest rate) au ni riba isiyobadilika kulingana na kiwango cha mkopo kilichobakia(flat method)
Kujua hivi vitu ni muhimu sana itakusaidia usifanye maamuzi ya kuchukua mkopo kwa mihemko.
Kuna taasisi au wakopeshaji wenye riba kubwa sana kama huelewi hili unaweza kujikuta muda mwingi unautumia katika kulipa mkopo mkubwa sana kwa waliokukopesha.
Je andiko hilo limekusaidia? Kama limekusaidia basi usisite kutoa maoni yako na pia fuatilia page zetu za mitandao ya kijamii kwa jina la Mchumi Consulting.
IMEANDIKWA NA
Paul Mchumi
0714260266
Maoni
Chapisha Maoni