YAFAHAMU MAMBO 5 (MATANO) ILI KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO


Dunia ya biashara imekua ikibadilika mara kwa mara,hii ikiwa ni pamoja na ujuzi au mikakati mbalimbali ambayo imekua ikitumika kulingana na aina ya biashara husika nayo huwa inabadilika.

Haijalishi kama ndio unaanza biashara au ni mzoefu kwenye biashara fulani itakulazimu kuendana tu na mabadiliko mbalimbali ili uweze kufanikiwa kibiashara.


 Katika andiko hili tutashirikishana mambo kama matano muhimu ili kusaidia kufanya biashara yenye mafanikio ili uweze kutimiza malengo yako uliyojiwekea.


1.JENGA JINA(BUILD A BRAND)

Brand ni zaidi ya nembo ya biashara yako. 

Huu ni utambulisho wa biashara yako na kwa namna gani unafikisha utambulisho huo kwa wateja wako.


Ukiwa na brand(jina) kubwa ni rahisi kuwa mbele ya washindani wako,na vilevile utavutia watu wengine waje kwako na pia utaongeza thamani yako sokoni.

 

Hivyo ni muhimu sana ukaweka mikakati ya kujenga brand yako kwa kujitofutisha na washindani wako kwa kuwapa wateja bidhaa au huduma tofauti na washindani wako.

Pia tengenenza utambulisho wako wa kipekee ambao wateja watakutambua kupitia utambulisho huo,hapa tunazungumzia vitu muhimu kama jina la biashara yako,chapa(logo yako),rangi unazotumia,sauti n.k


Ni muhimu pia ukawa na mikakati mbalimbali ili kukuza jina lako(brand) sokoni,kama vile kujitofautisha na washindani wako,namna gani unahudumia au kuuza,pia kuwa na vitu vya ziada ambavyo ni muhimu kukuweka mbele ya washindani,hii itakusaidia zaidi kuacha kumbukumbu isiyofutika kwa wateja wako.


2. FAHAMU WATEJA WAKO

Ni muhimu sana kufahamu wateja wako unaowauzia au unaowapa huduma yako. Hapa ni muhimu kufahamu hawa wateja wanataka nini,mahitaji yao ni yapi na yapi,na wana tabia gani.


Hii itakusaidia zaidi kuwa na bidhaa au kutoa huduma ambazo zitatatua matatizo na changamoto zao mbalimbali na kurahisisha zaidi utoaji wa huduma kwao.


Unaweza ukafahamu mahitaji ya wateja wako na nini wanahitaji zaidi kwa kufanya utafiti kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kuangalia washindani wako wanafanyaje na mbinu nyingine nyingi.


3. KUWA NA MUENDELEZO (BE CONSISTENT)

Muendelezo wa huduma zako ni nguzo muhimu sana ya kujenga uaminifu na heshima uliyo nayo kwa wateja wako. Unatakiwa utimize unacho ahidi siku zote(deliver on your promises)


Na pia muendelezo huwa unasaidia kutengenenza wateja wale ambao watakua nawe kipindi chote na hawa watakusaidia zaidi hata kukutafutia wateja wengine huko mbeleni.


Hivyo ni muhimu sana ukaboresha huduma zako na kuongeza thamani. 

Pamoja na kuwasikiliza wateja wako wanataka nini,ili ujue wapi panahitaji kuboreshwa zaidi.

4. ZINGATIA WAFANYAKAZI WAKO

Timu yako kwenye biashara(watu unaofanya nao kazi) ni nguzo muhimu sana. 

Ni muhimu ukaajiri watu/wafanyakazi ambao ni sahihi,waelekeze namna ya kufanya kazi inavyotakiwa,wahamasishe ili waipende kazi yako.


 Wafanyakazi wenye furaha huwa wanakusaidia kufikia malengo ya kibiashara kiurahisi zaidi.


Na ukiwafanya wafanya kazi wako waipende kazi itakusaidia kubaki nao kwa muda mrefu na wafanyakazi ambao ni wazalishaji wazuri na itakusaidia kupunguza gharama za kutafuta wafanyakazi wengine na kuanza upya kuwaelekeza kazi.


5. PATIKANA KIURAHISI

Wateja huwa wanapenda waweze kukupata kiurahisi zaidi au kuifikia biashara yako kiurahisi. 


Tengenenza mifumo mirahisi ya upatikanaji wako kama ni kwa njia za simu,email,au mitandao ya kijamii.

Ukipatikana kiurahisi inajenga mahusiano mazuri na wateja wako na inaongeza uaminifu zaidi. 


Patikana,sikiliza na kuwa na njia zaidi ya moja ya upatikanaji wako.


Je andiko hili limekusaidia?

Kama andiko hili limekusaidia basi usisite kutoa maoni yako na kufuatilia kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii kwa jina la Mchumi Consulting.


IMEANDIKWA NA

Mchumi Consulting

0714260266

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA