MFAHAMU PAUL CHENGULA

 MFAHAMU PAUL CHENGULA


Karibu katika ukurasa wangu! 

Naitwa Paul Chengula, maarufu kama Paul Mchumi
Mimi ni mwanataaluma mwenye shauku ya kuona mabadiliko ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na biashara nchini Tanzania. 

Kwa zaidi ya miaka kumi,mpaka sasa nimekuwa nikifanya kazi katika taasisi za Fedha na Benki mbalimbali Tanzania, nikichanganya utaalamu wa kibenki na mbinu za kisasa za kidijitali kusaidia jamii kukuza kipato.

Safari ya Kitaaluma na Uzoefu kwenye Taasisi za Fedha 



Safari yangu ya kitaaluma ilianzia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo nilihitimu Shahada ya Uchumi (Bachelor of Economics) mwaka 2012. 

Tangu wakati huo, nimejitolea kikamilifu katika sekta ya kibenki nchini Tanzania, nikiwa nimehudumu katika idara mbalimbali kwa zaidi ya miaka 10 mpaka sasa.

Uzoefu wangu mkubwa upo katika masuala Mikopo na usimamizi wa Mikopo(Credit Matters). 

Nimepata fursa ya kusaidia maelfu ya wateja kupata suluhisho la mitaji, kuelewa vigezo vya kukopesheka, na kusimamia mikopo yao kwa tija. 

Kupitia uzoefu huu wa zaidi ya miaka 10, nimejifunza kuwa changamoto kubwa ya watu wengi si kukosa fedha pekee, bali ni kukosa elimu sahihi ya jinsi mfumo wa kibenki unavyofanya kazi.

Uandishi na Elimu ya Fedha
Ukiachana na kufanya kazi katika taasisi za Fedha Tanzania kwa zaidi ya miaka 10 mpaka sasa na kama mchumi, naamini katika nguvu ya maarifa. 

Tangu mwaka 2024, nimejikita katika uandishi wa vitabu ili kuwafikia watu wengi zaidi nje ya kuta za ofisi za Taasisi za kifedha. Mimi ni mwandishi wa vitabu viwili muhimu:


  "Kuza Uchumi Wako Sasa": Katika kitabu hiki, nimeainisha mikakati madhubuti ya kukuza uchumi binafsi (Personal Finance).
 Ni mwongozo kwa kila mtu anayetaka kutoka hatua moja ya kifedha kwenda nyingine.






 "Misingi ya Uwekezaji": Hapa nimeelezea kwa undani kanuni za uwekezaji katika masoko ya mitaji. Nazungumzia jinsi ya kuwekeza kwenye Shares (Hisa), Bonds (Dhamana za Serikali), na mifuko ya uwekezaji wa pamoja (Collective Investment Schemes).

Lengo langu ni kufanya mada ngumu za kiuchumi kuwa rahisi kueleweka kwa kila Mtanzania ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kifedha.







Mapinduzi ya Masoko ya kidijitali na Biashara

Pamoja na kuwa na majukumu ya kibenki ya muda wote (Full-time Banker), nimebobea pia katika Digital Marketing.
 
Nimegundua kuwa dunia ya sasa inahamia mtandaoni, na biashara nyingi nchini Tanzania zinahitaji daraja la kuzifikisha kwa wateja.

Nimefanikiwa kusaidia zaidi ya wafanyabiashara 500 nchini Tanzania kupata wateja na kukuza mauzo kupitia:

 Social Media Management: Kusimamia kurasa za biashara kitaalamu.

 Social Media Promoting: Kufanya matangazo yenye kulenga wateja sahihi (Targeted Ads).

 Lead Generation: Kutengeneza mifumo inayovuta wateja wapya kila siku.
Hii ni huduma ninayoifanya kwa mapenzi makubwa (privately), nikiamini kuwa teknolojia ndiyo njia rahisi ya kukuza biashara ndogo na za kati (SMEs).




Huduma za Ushauri (Consultation)
Leo hii, Paul Mchumi amekuwa kimbilio kwa watu wanaohitaji ushauri wa kitaalamu katika maeneo yafuatayo:

✅ Investment Consultation: Wapi uwekeze fedha zako ili zipate faida kubwa na usalama?

 ✅ Finance & Economics: Uchambuzi wa mwenendo wa uchumi na athari zake kwenye biashara yako.

 ✅Marketing & Branding: Jinsi ya kuifanya biashara yako iwe na jina kubwa na ivutie wateja.

Mimi nipo hapa kuwa daraja lako kuelekea mafanikio yako mbalimbali .Naamini katika uadilifu, weledi, na matokeo yanayoonekana.





Wasiliana Nami Leo:
Je, unahitaji mwongozo wa uwekezaji? Au unataka kukuza biashara yako kidijitali? Tuwasiliane:

 Jina: Paul Chengula (Paul Mchumi)
 Simu/WhatsApp: 0714 260266

FAHAMU ZAIDI KUHUSU MIMI HAPO CHINI 

BONYEZA LINKπŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

BONYEZA HAPA ILI KUMFAHAMU ZAIDI PAUL


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA