MAMBO HAYA 5 YANAMALIZA FEDHA ZAKO
Hivi umewahi jiuliza ni kwanini mtu fulani anapokea kipato kikubwa sana kama ni kazini au ofisi fulani au ana biashara ina mauzo makubwa sana,lakini mtu huyo kila siku anahangaika na madeni,au shida za pesa za hapa na pale.
Kumbuka pesa huwa inahitaji nidhamu na huwa inahitaji heshima,kwa maana ya kwamba ukiiheshimu na kuwa na nidhamu nayo huwa inakaa kwako.
Lakini ukii-treat vibaya nayo huwa inaondoka inakwenda kwa yule anaeipa heshima na kui-treat vizuri
Kuna baadhi ya mambo ukiyaendekeza au ukiwa unayafanya mara nyingi inakua ni mara chache sana kubakia na pesa,na utajikuta kila siku unatafuta mchawi ni nani anaesababisha usifikie malengo fulani kwenye maisha yako. Leo tumeorodhesha mambo matano yanayotafuna pesa zako kimya kimya na wewe umekua ukiyachukulia kawaida
1. Matumizi kwenye vitu visivyo na ulazima
Hili limekua ni eneo linalotafuna pesa za watu wengi sana,pale ambapo mtu unajikuta unaingia kwenye matumizi ya kununua vitu ambavyo hukupanga na havina ulazima sana,mfano umetoka nyumbani kwenda zako mjini huna bajeti ya kununua chochote,lakini huko mjini unakutana na kiatu au kitu fulani cha thamani unanunua.
Matumizi kwenye vitua ambavyo hukupanga huwa tunaita manunuzi ya mhemko(impulse purchase),amabapo unawiwa kununua kitu hata hukupanga na wala huna bajeti ya hicho kitu.
Sasa ni muhimu kuishi ndani ya bajeti yako,na kama unatoka hakiksha basi unatoka na kiasi fulani tu cha pesa na ujifunze kusema “no” kwa baadhi ya vitu au matumizi fulani fulani,hii itasaidia kutunza kiasi kiku bwa cha pesa yako,dhibiti sasa matumizi yasio na lazima kama kuenda na fasheni mpya kila siku,matumizi ya mabando makubwa ya simu,kulipia chanell za Tv usizotumia n.k
2. Starehe kupita kiasi
Hatukatai kuna muda mwili na akili ya binadamu huwa inahitaji kupumzika na kujiliwaza kidogo baada ya kazi au kujipongeza kwa ajili ya kitu fulani,hivyo kuna muda huwa unahitaji kupata starehe kidogo.
Hapa tunazungumzia zile starehe kupita kiasi,yaani kuna wale watu wao kuanzia jumatatu mpaka jumapili wao ni kula starehe tena za gaharama kubwa
Hii itakula pesa zako na itakurudisha nyuma sana kimaendeleo na kuna baadhi ya ndoto kwenye maisha yako itakua ngumu sana kuzifikia.
Kama ni starehe fanya kwa kiasi na kwa tahadhari kuhusu pesa yako na usizidishe sana,itasaidia kiasi kikubwa cha pesa usevu na kitaenda kwenye malengo yako ya uwekezaji au mambo mengine ya dharula yanayohitaji uwepo wa pesa yako
3. Mikopo mibaya
Kuwa na mkopo sio shida shida ni aina gani ya mkopo ulio nao,je mkopo wako ni kwaajili ya uzalishaji au mkopo wako ni kwaajili ya shughuli binafsi.
Kuna watu huwa wanaenda kwenye taasisi za kifedha au kwa watu binafsi wanachukua mkopo wenye riba kwa ajili ya matumizi yao binafsi yasiyo ya uzalishaji.
Kumbuka mkopo huwa unatolewa kwa riba maalumu,ambayo hiyo riba ndio gharama ya ziada unayoingi,mfano umechukua mkopo wa tsh 20,000/= ukaambiwa huo mkopo utarudi na elfu 5 ya ziada inamaana inatakiwa katika uzalishaji wako,uzalishe upate kurudisha pesa ya watu pamoja na ziada ambayo ndio riba
Sasa fikiria umechukua mkopo ukaenda kupeleka katika shughuli isiyo ya uzalishaji,huo mkopo utakupa gharama za ziada tu,na wengine huwa wanakua na mikopo mingi sana kila sehemu yupo,kila taasisi yupo(multiple loans),mwishowe mikopo inamzidi na anaishia muda mwingi kulipa mikopo ya watu na taasisi hivyo pesa nyingi inalika.
Anza sasa kujiwekea kipimo cha kiwango cha mikopo ya kuchukua na pia,hakikisha pesa ya mkopo unaipeleka kwenye uzalishaji.
4. Kujihusisha kwenye michango mingi
Hii sababu huwa inaonekana ya kawaida hasa kwa nchi yenye asili ya ujamaa kama Tanzania,na ukilisema hili,watu wanafikiria unataka uvunje mahusiano ya watu ya kijamii. Sasa fikiria wewe huyo huyo kwa mwezi una mchango wa harusi,sendoff,kipaimara,mchango wa kufa na kuzikana,mchango wa kikoba,mchango wa dawati shuleni,mchango kwenye group la wasap n.k
Kwa unavofikiria hapo wewe utabaki na pesa hata kama unazo nyingi?,yes kuna wale ambao wana kipato kikubwa sana wanaweza kufanya hivyo,lakini pia hulka ya binadamu ni kua ukiwa na pesa nyingi na matumizi pia huwa yanaongezeka.
Hivyo hata ukiwa na kipato kikubwa lakini ukishindwa namna ya kuepuka baadhi ya matumizi yasiyo na tija pesa zitalika pia
Sasa anza leo kuwa na kiwango na kipimo(threshold) ya kutoa kwenye aina fulani fulani ya michango,na baadhi ya michango unaweza achana nayo na isiharibu mahusiano na wenzio kwa kiasi kikubwa,uamuzi ni wako,ila jua eneo hili huwa linakula sana pesa za watu.
5. Maisha zaidi ya kipato
Kila mtu huwa anahitaji maisha mazuri,na miongoni mwa mahitaji ya kila binadamu huwa kuishi maisha mazuri hilo hitaji lipo,lakini je unaishi maisha mazuri ya aina gani. Kuishi maisha yaliyo juu ya kipato chako unachoingiza lazima itakugharimu sana maana pesa nyingi itatumika ku-finance hiyo lifestyle ya juu uliyoichagua
Kuna watu wana kipato cha kawaida lakini huwa wanafosi kuishi maisha ya juu sana,unakuta nyumba anayoishi ni ya gharama sana,gari expensive anashindwa hata kuli-accomodate n.k. Wengine wanaishi maisha ya gharama ili kuridhisha majirani,ndugu,jamaa na marafiki lakini kimsingi maisha hayo yanakula sana akiba zake.
Anza sasa kupunguza baadhi ya gharama na kuachana na maisha fulani ambayo sio yako kwa sasa,unaweza ishi leo maisha standard kabisa wakati pesa hiyo nyingine unasevu au unaekeza kwenye mambo mengine ambayo ni productive na baadae ukiwa na kipato kikubwa utaishi maisha hayo unayoyatamani.
Hii ni ngumu kumeza kwa watu wengi,maana huwa tunafosi sana maisha ya juu wakati kipato ni cha chini.
IMEANDIKWA NA
Mchumi Consulting
0714260266
👇👇
Maoni
Chapisha Maoni