SABABU SITA(6) ZA KWANINI WATEJA HAWANUNUNI BIDHAA AU HUDUMA YAKO
Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kufanya mteja asifanye maamuzi ya kununua kile unachouza.
Tumeelezea sababu 6 kiundani hapa chini,na ni namna
gani unatakiwa ufanye ili uweze kumnasa mteja na anunue unachouza
1.KUTOKUONA THAMANI(BEI KUBWA)
Hapa mteja huwa analinganisha BEI ya
bidhaa na thamani anayoipata kutoka kwenye bidhaa au huduma yako.
Pindi mteja kichwani mwake akifikiria
kuwa thamani ni ndogo kuliko bei basi jua hatanunua kitu chako.
Zingatia kumuelewesha mteja aone
thamani anayopata ni kubwa kuliko bei ya bidhaa yako.
2. HAKUAMINI(LACK OF TRUST)
Hii ni sababu kubwa inayofanya
wafanyabiashara wengi kushindwa kuuza bidhaa au huduma zao.
Kama mteja haiamini brand yako jua
utapata changamoto sana.
Kukosekana kwa uwazi(transparency)
juu ya kile unachokiuza jua inaweza kusababisha mteja atapate wasiwasi mkubwa.
Weka nguvu kubwa katika kujenga
jina(brand) na kuwa na shuhuda nzuri za wateja uliowahi kuwauzia bidhaa au
huduma yako
Kuna watu wanauza bidhaa za kawaida
sana na wanapata wateja wengi kwa sababu tu wana brand(jina) kubwa.
3. KUTOKUONA UHITAJI WA UNACHOUZA
Kama mteja haoni umuhimu au hana
uhitaji wa kile unachouza kwa sasa ni wazi jua huyo mteja hatanunua.
Usikasilike pindi mteja hanunui kile
unachouza huenda unauza kitu ambacho yeye haoni umuhimu wa kuwa nacho kwa sasa.
Au huenda bidhaa au huduma yako haikidhi mahitaji ya mteja anayohitaji kwa wakati huo.
Ni vizuri kufahamu aina ya wateja
unaowatageti wanahitaji bidhaa au huduma ipi,hivyo usiuze vitu kwa sababu wewe
unavipenda ila angalia uhitaji wa wateja.
4. KUKOSEKANA TAARIFA ZA KUTOSHA
Wateja huwa wanataka wawe na taarifa
za kutosha juu ya bidhaa unayouza ili wasikosee kufanya maamuzi ya kununua.
Kama mteja hataelewa faida atakayoipata kutoka kwenye bidhaa yako jua ni ngumu kununua unachouza.
Hivyo wekeza nguvu kubwa kutoa
taarifa za faida zilizopo kwenye bidhaa unayouza ili umrahisishie mteja kufanya
maamuzi ya kununua.
5. USHINDANI WA KISOKO
Kama endapo kuna washindani wengine wanaouza bidhaa au huduma kama yako lakini ina thamani kubwa au bei ya chini zaidi yako jua hawatanunua kwako.
Vilevile kama mshindani wako ana jina
kubwa(brand) zaidi yako na anauza bidhaa au huduma kama yako basi jua mteja
ataenda kwa mshindani wako.
Sasa jiongeze kutoa huduma nzuri na
haraka zaidi ya mshindani wako ili mteja aone umuhimu wa kununua kwako na si
kule.
6. UNAKOSA MIKAKATI YA USHAWISHI
Kujua namna ya kumshawishi mteja ni
jambo la lazima ambalo mfanyabiashara unatakiwa ujue.
Usipoweza kushawishi jua hufai kuwa
mfanyabiashara.
Jua mikakati mbalimbali ya kufanya
masoko na kuwasiliana na mteja.
Fahamu lugha nzuri za kumhamasisha mteja kununua
sasa na sio siku nyingine.
Weka kila aina ya ushawishi wa
kumvuta mteja kwako na sio aende sehemu nyingine.
Huduma nzuri na za haraka ni jambo
jingine la msingi kuzingatia ili uweze kumshawishi mteja anunue kwako n.k
Wekeza pia katika promotion na kujitangaza
zaidi.
Hizi ni baadhi tu ya sababu lakini
kuna sababu nyingine nyingi zinazoweza sababisha mtu asinunue unachouza kama hali yake
ya kiuchumi,kuwa na wasiwasi juu ya unachouza na sababu nyingine nyingi.
TAZAMA HUDUMA ZETU NYINGINE HAPA
IMEANDIKWA NA
Mchumi Consulting
0714260266

Maoni
Chapisha Maoni