NINI MAANA NA FAIDA YA KUIFANYA BIASHARA YAKO KUWA KAMPUNI


Kampuni ni chombo cha kisheria  kinachoundwa na watu wawili au zaidi kwa nia ya kuendesha biashara au shuguhuli nyingine yoyote ya kiuchumi au kijamii. Kwa Tanzania mamlaka inayosimamia usajili wa makampuni ni BRELA chini ya sheria ya Makampuni ya mwaka 2002.


Kampuni ina uwepo wa kisheria  tofauti na wamiliki au wanahisa wa kampuni husika. Vilevile Kampuni inaweza kumiliki mali,kuingia mikataba,kushitaki au kushitakiwa na kulipa kodi kwa kutumia jina lake.

Kuna faida nyingi sana ambazo zinapatikana kama endapo utaamua kuifanya biashara yako iwe katika mfumo wa kampuni tofauti na ikiwa katika mfumo wa kawaida wa jina la biashara. Na katika andiko letu tutaelezea baadhi ya faida zinazopatikana ambazo utazipata tu pale ukiisajili biashara yako katika mfumo wa kampuni.


1.Faida upande wa kodi(Tax benefits)

Miongoni mwa faida unayopata ukiwa umesajili biashara katika mfumo wa kamapuni ni upande wa kodi unayolipa.

Mara nyingi kampuni huwa zinalipa kodi kutoka kwenye faida iliyopatikana ndani ya kipindi fulani.


Hivyo kulingana na kiwango chako cha mapato na aina ya kampuni,utajikuta unalipa kodi ndogo kuliko ukiwa mtu binafsi.

Kwa mfano kwa Tanzania kodi za makapuni ni 30% kwa sasa wakati kodi kwa biashara ambayo haipo katika mfumo wa kampuni au mtu binafsi inaweza kuwa zaidi ya asilimia 30% kulingana na mapato husika.


Na vile vile ni rahisi kuomba punguzo la kodi katika mamalaka husika kutokana na gharama mbalimbali ambazo kampuni imeingia kulingana na uataratibu uliowekwa kisheria na kusimamiwa na mamlaka husika za kodi.


2. Heshima na kuaminika(Credibility and reputation)

Ukisajili biashara yako katika mfumo wa kampuni huwa unaipa biashara heshima na kuaminika zaidi.

Wateja na wadau wengine huwa wanaamini zaidi biashara zilizosajiliwa katika mfumo wa kampuni kuliko biashara ikiwa kawaida.

Na kuna baadhi ya dhabuni ni rahisi kupata kama endapo biashara ipo katika mfumo wa kampuni kuliko ikiwa kawaida.


Kusajili biashara katika mfumo wa kampuni huwa kunavutia wateja na wadau wengine wengi na kuongeza mauzo na faida kwa ujumla

Vilevile biashara ikiwa imesajiliwa katika mfumo wa kampuni huwa inalinda kisheria watu wengine wasitumie jina au mali  nyingine bila ruhusa ya kampuni(brand identity)


3. Urahisi wa kupata na kuongeza mtaji(Access to capital)

Miongoni mwa faida zinazopatika kama endapo biashara ipo katika mfumo wa kampuni ni pamoja na urahisi wa kupata na kukuza mtaji.


Kama kampuni huwa ina uwezo wa kuongeza mtaji wake kwa kuuza hisa kwa wawekezaji mbalimbali ambapo zikiuzwa kampuni huwa inaongeza mtaji wake tofauti na biashara ikiwa kawaida haiwezi kuvutia wawekezaji kwa kiasi kikubwa. Lakini pia kampuni inaweza kupata na kuongeza mtaji wake kwa kukopa fedha kutoka benki au taasisi nyingine za kifedha.


Kama inavyojulikana kuwa kampuni inao uwezo wa kukopa na kupata fedha kwa kutumia jina lake.

Hivyo kwa kuwa inao uwezo wa kupata na kuongeza mtaji kwa njia ya kuuza hisa au kukopa inaweza ikaongeza mtaji na kuweza kutimiza majukumu mengine ya kikampuni kiurahisi kama kukuza biashara,kuwekeza katika teknlojia au mashine fulani au hata kuingia kwenye soko jipya.


4.Umilele na urahisi wa kuhamisha(perpetuity and transferability)

Faida nyingine inayopatikana kwenye kampuni ni urahisi wa kuhamishisha na muendelezo wa biashara(umilele).

Tofauti na biashara binafsi kampuni huwa haifi pale ambapo muazilishi/mmiliki amefariki au amestaafu au ameachana nayo.


Kampuni huendelea kuwepo mpaka pale itakapoamuliwa kuvunjwa rasmi kisheria na wanahisa au pale endapo itaungana na kampuni nyingine(merge)

Ndio maana mpaka leo kuna baadhi ya kampuni zipo na zinaendelea kuwepo ingawa waanzilishi na wamiliki wake hawapo duniani kwa sasa.


Hii ina maana chombo ulicho kianzisha kitaendelea kubaki hata kama umefariki.

Lakini vilevile ni rahisi kuhamisha umiliki wa wahusika/wamiliki wa kampuni kwa mtu mwingine kwa kumuuzia au kumuhamishia hisa za kampuni maana hiyo ipo kulingana na utaratibu na matakwa ya kisheria.


Utaratibu huu wa kuhamisha au kuuza hisa huwa unakupa wewe mmilikia au mwanahisa urahisi zaidi pale unapotaka kuachana na kampuni au kustaafu maana utahamisha au kuuza hisa zako kwa watu wengine unaoona wanafaa.


5. Kujulikana kisheria (legal recognition)

Miongoni mwa faida nyingine ya kuisajili biashara yako iwe katika mfumo wa kampuni ni kuwa itapata kujulikana kisheria na kupata kinga na haki mbalimbali.


Kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania huwa inapata uwezo na utu wa kisheria ambapo inaweza kumiliki jina,mali mbalimbali zinazokua chini ya jina lake,vile vile  kampuni inaweza kushitaki au kushitakiwa yenyewe kwa jina lake.

Hii husaidia zaidi kisheria na hasa haki anazopata mmilikia au mwanahisa wa kampuni fulani kwani kuna haki za kisheria anafaidika nazo kama endapo tu biashara ipo katika mfumo wa kampuni.


Kuna mazingira yanaweza kujitokeza ambapo inayoshitakiwa ni kampuni na wala sio mmilikia au mwanahisa,maana kampuni ina utu wa kisheria na inaweza kushitakiwa ama kushitaki.

Na pia kuna mazingira ya kisheria yanayokupa wewe mmiliki ahueni ya kisheria hasa upande wa mali unazomiliki huwa haziguswi kisheria pale ambapo imetokea kunahitajika kulipwa deni fulani la kampuni na wadai wanahitaji kupata fidia ya deni lao au deni husika kulipwa.


Wewe mmiliki au mwanahisa mali zako binafsi nje ya kmapuni huwa haziguswi au kuchukuliwa ila madai yatahusu mali zinazomilikiwa na kampuni tu tofauti na ukiwa unamiliki biashara isiyo kampuni mali zako binafsi zinaweza kuchukuliwa kama kuna deni linatakiwa lilipwe kulingana na matakwa ya kisheria.


Hizo ni baadhi tu ya faida zinazopatikana pale tu utakapoisajili biashara yako katika mfumo wa kampuni.

Lakini kuna gharama kadhaa ambazo zinaambatana  pale unapoifanya biashara yako katika mfumo wa kampuni kama vile ada za usajili wa kampuni unazoingia wakati wa kusajili,vilevile utapaswa uanze kufuata matakwa ya kisheria kama kutengenenza ripoti za kila mwaka za mahesabu ya kumpuni,rekodi za ukaguzi na kihasibu.

Hivyo kabla hujaamua kusajili biashara yako katika mfumo wa kampuni ni muhimu pia ukaangalia na kupima faida na gharama zipi utaingia na utakazo paswa kufuata kabla na baada ya kuanzisha kampuni.

IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA:

MCHUMI CONSULTING

0769 218125/0714 260266(WhatsApp)

MFANYABIASHARA JIUNGE BURE NA GROUP LETU LA WASAP ILI KUPATA HUDUMA NA MASOMO YETU MUDA WOTE👇👇

BONYEZA HAPA KUJIUNGA BURE NA GROUP LETU LA WASAP


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

REDUCING LOAN DEFAULTS: Proven Methods for Tanzanian Banks and Financial Institutions

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA

Tech and Transactions: The Rise of Selcom Pesa and Its Impact on Tanzania's Economy