SABABU 9 ZA KUZUIWA AKAUNTI YA KURUSHA TANGAZO LAKO KUKATALIWA MTANDAONI(FACEBOOK/INSTAGRAM)



Mitandao ya kijamii imekua msaada mkubwa sana wa kuzikutanisha biashara na wateja mbalimbali hivi sasa. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii imekua maarufu sana siku hizi kwa ajili ya wafanyabiashara kutangaza bidhaa au huduma zao.

Mitandao ya kijamii kama Instagram,Facebook,Tweeter na mingineyo imekua njia mojawapo ya pendwa sana ya kufanyia biashara. 


Uzuri wa kutangaza biashara kupitia mitandao ya kijamii ni kuwa unakutana na watu wengi(audience) kwa gharama ndogo sana.

Sasa ili uweze kufanya matangazo ya kulipia mitandaoni kama Facebook au Instagram utapaswa uwe na akaunti maalumu zilizo katika sifa ya kufanyia biashara(business account). 

Na uzuri ni kwamba hata akauti yako ya kawaida ya Facebook au Instagram au tweeter unaweza ukaifanya ikawa na uwezo wa kufanya matangazo ya kulipia(business account)


Unaweza pia ukafanya matangazo ya kulipia kupitia google au youtube ambapo utatakiwa kujiunga na kurusha matangazo kupitia google ads. 

Kwa upande wa matangazo ya google yenyewe unaweza kutangaza bidhaa au huduma zako kupitia youtube au ukatangaza vitu vyako vikaonekana kiurahisi katika search engine ya google na mwisho utapata kujulikana na watu wataona kile unachotangaza.


Hii ni fursa kwa mfanyabiashara na unatakiwa usiichukulie kawaida maana mifumo ya kisasa inakulazimisha ukutanishe biashara yako na watu mbalimbali kupitia mitandao. 

Sasa katika andiko hili tutaona ni mambo gani yanaweza fanya akaunti yako ya kurusha matangazo kufungwa au tangazo ulilorusha la bidhaa au huduma kukataliwa.


Na tutaangalia kiundani zaidi hasa mitandao miwili maarufu ya Facebook na Instagram maana imekua maarufu sana kujitangaza kwa mfumo wa kulipia Na kama endapo utakutana na tatizo la kufungwa akaunti yako au tangazo lako kuzuiwa kipi unatakiwa ufanye ili tatizo hilo lisijirudie tena.


1. Kuvunja sera ya matangazo(policy violation)

Miongoni mwa sababu ya kuzuiwa tangazo lako au kufungwa kwa akaunti ya matangazo(Facebook/Instagram) ni pamoja na kukiuka sera za urushaji wa matangazo .Kimsingi unapaswa uelewe na usome kiundani sera za namna ya kurusha matangazo ya kulipia ambazo kila mtandao huwa inakua nazo.
Mitandao yote huwa ina sera maalumu za kujitangaza na namna ya kufanya ukiwa unafanya matangazo mitandaoni. 


Tangazo lako likizuiwa kwa sababau ya uvunjifu wa sera kipengele fulani utajulishwa kwa email au kupitia akaunti husika kuwa tangazo lako limezuiwa au akaunti yako imefungwa kwasababu imekiuka sera za utangazaji na unaweza ambiwa kabisa sera ipi iliyovunjwa.


Hivyo ni muhimu kupitia sera ya utangazaji wa bidhaa au huduma Facebook au Instagram ili ujue vitu gani huwa vinakatazwa. 
Na mara nyingi tangazo lako likizuiwa kwasababu ya kukiuka sera za matangazo huwa unapewa fursa ya kukata rufaa(review),ni muhimu kutumia fursa hii kwani mara nyingine system huwa zinakosea. 
Na kama endapo system zilizuia akaunti kimakosa basi tangazo au akaunti huwa inarudishwa kawaida na kuendelea kuwa hewani


Sera zipi ukivunja tangazo huzuiwa au akaunti hufungwa?

Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vinavyokatazwa kutangazwa na endapo system za facebook au Instagram zikigundua basi tangazo lako huzuiwa
  • Madawa ya kulevya na aina nyingine za vilevi vyenye madhara.
  • Kutangaza maudhui ya kibaguzi kwa jamii fulani au vitendo vyovyote vya kibaguzi(discriminatory practices) Kama “njoo ukutane na watu Weusi hapa”,”njoo upone kisukari chako”au “waisilamu hawa wamevunja rekodi”n.k
  • Aina fulani za silaha za maangamizi
  • Picha au video zinazoonyesha utupu wa binadamu
  • Site za kimapenzi ambazo hazijaruhusiwa
  • Picha zinazoonyesha matokeo yasiyo ya kawaida ndani ya muda mfupi(picha za before and after)
  • Matendo yoyote ambayo yanaonyesha kujipatia fedha katika mfumo ambao sio wa kawaida(utajiri wa haraka)
  • Matendo ya kujidhuru au kudhuru wengine (kujinyonga n.k)
  • Huduma na aina fulani za michezo ya bahati nasibu na kamali
  • Matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku
  • Matangazo kuhusiana na uchaguzi,siasa au ajira bila kibali maalumu.
  • Sababu nyingine nyingi.

2. Kutofanyika kwa malipo ya tangazo(payment failure)

Hii ni sababu nyingine inayoweza kufanya akaunti yako kuzuiwa au tangazo ulirusha kushindwa kukubaliwa. Kuna mazingira hutokea ambapo huko nyuma huenda uliwahi rusha tangazo kwa kujua au kutojua na akaunti yako ikatakiwa kulipia tangazo husika lakini hukufanya malipo hayo.
Hivyo pale unapotakiwa kurusha tangazo jingine litakataliwa kwasababu kuna deni halikulipwa huko nyuma. 


Kuna aina ya mifumo ya ulipaji wa matangazo ambao huwa pesa inakatwa pale ambapo akaunti ikifikisha kiwango fulani kutokana na matakwa ya mhusika wa akaunti(payment threshold)
Mfano unajiwekea kuwa tangazo likate pesa kila nikifikia matumizi ya dola 10,hii ina maana tangazo lako likifikia dola 8 ukalizima au ukalisimamisha pesa itakua haijakatwa kwenye njia yako ya malipo kwani uliweka tangazo likate ikifikia dola 10. Na mwisho wa siku akaunti hiyo ukija kuitumia siku nyingine utatakiwa kulipa na deni la nyuma,ambalo inakua ni kama ulikopeshwa.


Lakini vilevile akaunti yako inaweza kuzuiwa kama endapo hakuna pesa za kutosha katika mfumo wako wa malipo na sytem inataka ikate pesa lakini inakuta hakuna kitu. 
Na sababu nyingine yoyote inayofanya malipo ya tangazo husika yasiweze kukatwa kutoka katika mfumo wako wa malipo kwa kujua au kutojua husababisha tangazo lako kuzuiwa kwenda hewani.


3. Kutumia vibaya logo ya Facebook na jina

Hili ni suala ambalo warushaji wengi wa matangazo huwa hawalijui. Matumizi ya neno “Facebook” ni muhimu kufahamu kuwa inatakiwa katika maandishi yako(caption) herufi ya kwanza iwe kubwa na usiandike kiufupi kama vile kuandika “FB” au “facebook” badala yake neno hilo inatakiwa lisomeke “Facebook”.


Vilevile inatakiwa uwe makini wakati wa kutumia logo ya Facebook au Instagram ,hata kama wewe ni mtaalamu wa kunyumbua logo hutakiwi kuweka logo yako inayofanana na ya Facebook au Instagram.


Hivyo hakikisha unatumia logo ya Facebook ambayo ni standard inayotumika na wao Facebook na si vinginevyo. Hii huwa sababu nyingine inayoweza fanya tangazo lako likazuiwa(rejected) kwa kutozingatia kitu kidogo kama hicho


4.Uandishi mbaya wa maneno(Caption)

Facebook au Instagram huwa hawataki tangazo lao lionekane kama la kitapeli(spammy). Kuna baadhi ya uandishi wa maneno ya post yako yanaweza fanya tangazo lako likakataliwa.

Matumizi kama ya herufi kubwa zote kwenye maelezo yako(caption) huwa hayaruhusiwi,lakini vilevile kutumia hamasa ya emoji nyingi badala ya maneno ili kupendezesha andiko lako nalo huwa hairuhusiwi. 


Vile vile kuchanganya changanya herufi na font kwenye post yako au kutumia hashtag nyingi kwenye post inaweza fanya tangazo lako likakataliwa.

Jitahidi kua na uandishi bora wa maelezo yenye mvuto na yaliyo katika mtiririko unaoeleweka(be professional). 


Acha mbwembwe nyingi pale unaporusha tangazo la kulipia ila hakikisha caption yako inakua yenye mvuto hata mtu akiona anaona hapa kweli huyu anaetangaza biashara hii yupo siriaz na anajielewa.

Acha kuandika maneno ya tangazo(caption) kama unakimbizwa,na acha kutumia ufupisho wa maneno.


5. Makosa ya tangazo linakoelekea(landing page)

Landing page ni eneo ambalo unataka tangazo lako watu waende inaweza kuwa ni kwenye website fulani au ukurasa wowote. 
System za Facebook au Instagram huwa zinaenda moja kwa moja mpaka unakotaka tangazo lako liwafikie watu.


Kwahiyo kama umeweka link fulani basi system zitacheki kama hiyo link inawapeleka watu kwenye page au website ambayo ni halali na haina mashaka yoyote ya utapeli au kitu chochote chenye kuumiza watu. 
Maana wengine wanaweza kurusha tangazo na kuweka link inayopeleka watu kwenye website yakitapeli nakadhalika.


Na pia unakotaka watu waende ni lazima kuwe kunaeleweka,kama ni website ni muhimu iwe na jina na inahusu nini,lakini pia iwe na email address,na namba za simu n.k. 
Ndio maana kama unataka urushe tangazo kwenda whatsap ni muhimu whatsap yako ikawa ni whatsap business maana huwa ina taarifa za kutosha za biashara yako na mambo inayo deal nayo.


Na vile tangazo linakoelekea(landing page)inabidi kuonyeshe uhalisia wa kitu unachotangaza kwenye tangazo lako kule Facebook au Instagram kiakisi uhalisia na kwenye page yako unakotaka wateja waje kwa ajili ya mazungumzo na maelekezo zaidi kama ni kwenye website,whatsap au site yoyote.


Sio kwenye Facebook au Instagram umetangaza kuwa unauza vifaa vya pikipiki lakini watu wakija whatsap au wakienda kwenye website yako wanakuta unauza dawa za nguvu za kiume hapo tangazo lako likigundulika litazuiwa.

Kwahiyo hakikisaha page au site unayotaka watu waende inabidi isiwe na dalili zozote za utapeli tapeli au udanganyifu na wizi wowote wa taarifa au fedha za watu.
Na vilevile hakikisha kama ni website basi inafikika kiurahisi sio unataka kuingia unatumia muda mrefu kuifikia website husika.


6. Akaunti kuwa au kuonyesha dalili mbaya(unusual activity)

Hiki ni kitendo ambacho system za Instagram au Facebook inakua ina kitafsiri kuwa kama kitendo ambacho sio cha kawaida au hujakifanya wewe. Kumbuka mitandaoni kuna watu huwa wanadukua akaunti za watu wengine(hackers)


Au wengine wanaweza kuseti system za kiroboti kwa ajili ya kufanya kazi fulani mitandaoni,na sera za utangazaji zinataka mhusika uwe kweli ni wewe binadamu halisi wala sio roboti. 

Lakini vilevile ili kuiweka akaunti yako katika hali ya usalama zaidi huwa system za Facebook au Instagram zinaizuia akaunti yako kwa ajili ya usalama wake.


Kuna matendo ukifanya sana au zaidi ya maramoja unalazimisha system zinahisi wewe ni mdukuaji hivyo zinafungia akaunti. 

Mfano unaweka taarifa zako za njia ya malipo(visacard au mastercard) unakosea kosea mara nyingi basi akaunti yako huwa inafungwa alafu watakuhitaji uthibitishe kama akaunti ni yako kwa kufanya verification.


Na vilevile kuna baadhi ya vitu vikifanyika system inahisi tu kuna kitu hakija kaa sawa kwenye akaunti yako na wewe bila kujua unakuta akaunti imefungwa na wanahitaji wajiridhishe kama wewe ndie mmiliki wa akaunti husika.


Ndio maana akaunti unayotumia kurushia matangazo hasa zile akaunti za Facebook(profile) inatakiwa jina liwe lako lililopo kwenye kitambulisho chako au aina nyingine ya uthibitisho wa majina yako.


Lakini kwa akaunti zile za biashara za Facebook(page) hakuna haja ya kuweka jina lako lililopo kwenye kitambulisho(ile unaweka jina la biashara au brand yako). 

Mara nyingi ikitokea tukio ambalo sio la kawaida huwa unapewa taarifa kuwa huwezi kurusha matangazo kwasababu akaunti yako imekutwa na tukio lisilo la kawaida


7. Kutoweka hatua za ziada za kiusalama(two factor authentication)

Pia kuna wakati akaunti inaweza zuiwa kufanya matangazo kwasababu hujaweka ulinzi wa ziada wa kiusalama kwenye akaunti husika.

Ukiachana na matakwa ya akaunti kuwa na password ya kuingilia,lakini unapaswa pia uiwekee akaunti yako ulinzi wa ziada.


Two factor authentication ni system ya kuongezea ulinzi wa ziada akaunti yako ili iwe vigumu mtu mwingine kuingia kwenye akaunti yako bila ruhusa yako.

Hapa unaseti namba ya simu au email au unatumia kitu tunaita backup code,au App fulani kwa ajili ya kuingia kwenye akaunti yako(login)


Lakini njia inayotumika sana hasa kwa Facebook ni kuweka namba ya simu ambayo code namba hutumwa pale tu mtu akitaka kuingia kwenye akaunti yako kwa kutumia kifaa kingine ambacho huna taarifa nacho na hukitambui na wewe utapewa taarifa(notification)

Hivyo utatumiwa ujumbe wa code namba kwenye simu yako kujiridhisha kama unamtambua huyo mtu ili utoe uthibitisho na ruhusa.


Sasa kama akaunti yako hujaunga huu mfumo ni rahisi kuzuiwa kwa ajili ya usalama wa akaunti husika.

Ndio maana kuna akaunti huwa zinaongoza kwa kufungwa na Facebook au Instagram lakini kuna nyingine hazifungwi mara nyingi ikiwemo sababu hii ya kiusalama ya two factor authentification.

Ni muhimu sasa ukaweka huu mfumo kwenye akaunti zako ili kuzilinda kiusalama zaidi na ili akaunti yako isifungwe mara nyingi pale inapotokea kosa hata dogo limefanyika.


8. Kama akaunti ni mpya.

Facebook au Instagrama wanaweza wakazuia akaunti yako kufanya matangazo hata kwa kosa dogo kwa sababu tu akaunti yako ni mpya. Kuna tofauti kati ya akaunti mpya na akaunti ya zamani iliyo katika mfumo wa kurusha matangazo.


Wanaamini akaunti mpya zinakua bado hazijakidhi vigezo vya kutosha kwa kufuata sheria zao. Ndio maana kuna baadhi ya vitu akaunti mpya haiwezi kuvifanya mapema lakini akaunti ya muda mrefu iliyofuata vigezo na sheria kwa muda mrefu huwa inaweza kuvifanya.


Na akaunti ikiwa mpya sana ikifanya kosa hata dogo ni rahisi kuzuiwa kwa ajili ya usalama wa akaunti. Hivyo ni muhimu kufuata sheria na sera za utangazaji ili akaunti yako ipewe daraja la juu na isifungwe mara nyingi.


9.Kuvunja sheria kwa kujirudia

Kuna wakati unaweza kuwa umevunja sheria na ukakata rufaa akaunti yako ikarudishwa au tangazo lako likarudi na kuendelea na matangazo. Lakini kuna muda inatokea labda umerusha tangazo limekataliwa kwa kukiuka sera au sheria za utangazaji,ukarudia kuweka tangazo lingine napo likakataliwa tena.


Basi jua kadri unavyovunja sheria na matangazo mengi kukataliwa ndio unaifanya akaunti yako kushushwa daraja(lowering account quality) na hii hufanya huko mbeleni tangazo jingine likataliwe pia kwani system huwa zinaamini na tangazo la sasa huenda limevunja sheria tena.


Na kama ukiendelea kuvunja sheria kwa kujirudia rudia ndani ya muda mfupi basi jua akaunti yako inaweza kufungwa kwasababu akaunti hiyo inaonekana ina shida.

Hivyo ukiona tangazo lako limekataliwa basi omba review au badilisha weka tangazo jingine lililofuata sheria na epuka kurudia kosa tena ili akaunti yako iendelee kuwa salama zaidi.

Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazoweza sababisha akaunti yako ya matangazo ikazuiwa kufanya mtangazo au tangazo ulilorusha kukataliwa.


Ni muhimu kufuata sera za kurusha matangazo zilizowekwa na Facebook/Instagram au aina nyingine ya mitandao ambayo ina huduma ya kurusha matangazo.

Na mara nyingi sheria za urushaji wa matangazo huwa zinafanana karibu kwa kila mtandao,huwa hazitoafautiani sana.

Kama biashara yako inategemea kwa kiasi fulani kupata wateja kutoka mitandaoni kwa kutumia matangazo ya kulipia ni muhimu kufuata sera hizi,na kuepeuka kila kitu ambacho kinaweza fanya akaunti yako kuzuiwa.


Je unazifahamu sababu nyingine za akaunti kufungwa au tangazo kuzuiwa au akaunti yako imezuiwa kufanya matangazo ya kulipia?

Wasiliana nasi tukushauri na tukusaidie kuirudisha ili uendelee kufanya matangazo zaidi kwa kutupigia simu au kwa whatsap kwa namba zetu za 0769 218125(voda) au 0714 260266(Tigo)


Imeandaliwa na kuandikwa na

Mchumi Consulting

Simu: 0769 218125

 MFANYABIASHARA JIUNGE BURE NA GROUP LETU LA WASAP ILI KUPATA HUDUMA NA MASOMO YETU MUDA WOTE
👇👇



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA