BIASHARA YAKO KAMA HAISIKIKI BASI HAKIKISHA INAONEKANA
Kikawaida akili ya binadamu huwa inasahau mambo kadhaa wa kadha kama endapo hayo mambo hayatumiki au hayaonekani.
Mfano huwa unapoteza ujuzi ulio nao kama endapo huutumii mara kwa mara.
Vilevile kuna baadhi ya vitu huwa unasahau kama huvioni mara kwa mara.
Hivi ndivyo biashara yako nayo itafanikiwa kama endapo watu wataendelea kuiona au kuikumbuka mara kwa mara.
Hapa tunazungumzia umuhimu wa KUITANGAZA BIASHARA YAKO siku zote.
Kamwe usifanye kosa la kuacha kuitangaza biashara yako.
Katika masoko kuna msemo unasema "Kama husikiki basi onekana,na kama huonekani basi sikika".
Mfano nikuulize ni lini imepita hujakutana na tangazo la soda ya 'cocacola'?
Cocacola ni soda ya enzi na enzi kila mtu anaijua lakini mpaka leo unaona wanaitangaza kwenye TV,redio, mtandaoni,magazetini n.k
Kwa ukubwa walio nao Cocacola wangeweza acha kuingia gharama ya matangazo,lakini wanajua umuhimu wa kuendelea kuonekana au kusikika.
Hata wewe hiyo bidhaa au huduma unayouza haitajulikana kama hutaipeleka machoni au masikioni kwa watu.
Kamwe usichukulie kawaida umuhimu wa kufanya matangazo ya biashara yako.
Na tena wewe mfanyabiashara wa zama za leo una bahati sana maana kuna mabadiliko ya kiteknolojia yapo upande wako.
Unaweza tangaza biashara yako kawaida au kupitia mitandao ya kijamii.
Haya sasa nakukumbusha nenda kafungue akaunti ya bidhaa au huduma yako mtandaoni hivi sasa kama huna.
Kama huwezi na hujui uanzie wapi kuitangaza biashara yako tupigie sisi Mchumi Consulting 0714260266 ili tukuelekeze na kukufundisha.
IMEANDIKWA na
Mchumi Consulting
0714260266
MFANYABIASHARA JIUNGE BURE NA GROUP LETU LA WASAP ILI UPATE MASOMO NA UPDATES ZETU MUDA WOTE
👇👇
Maoni
Chapisha Maoni