JINSI YA KUPUNGUZA GHARAMA ZA KUITANGAZA BIASHARA YAKO

Gharama za kupata wateja wapya zimekua zikiongezeka mara kwa mara.

Iwe ni unatangaza biashara yako kwa njia za kawaida(traditional) au unatumia njia za kisasa za fursa za kidijitali kote gharama ni kubwa.

Utatumia kwa siku kuanzia dola 4 ili kutangaza tangazo lako Instagram au Facebook ili watu wengi waone bidhaa yako.

Lakini gharama za matangazo ni kubwa zaidi hasa kwenye platforms nyingine kama Tweeter(X),youtube au Google.

Gharama za masoko ni kubwa hasa kwa wafanyabiashara wenye mitaji midogo.

Na kumbuka SIO ukitangaza biashara yako lazima upate wateja wanaonunua,kwani kuna muda unaishia kupata watu wanaouliza bei pekee bila kununua.

Hivyo ni muhimu kuwa na mikakati mingine ya ziada ya kupata wateja ukiachana na huu mkakati wa kulipia matangazo (sponsor) muda wote.

Kuwa na utaratibu wa kuwaomba wateja wako wakusaidie kukuongelea mazuri kwa wengine ili waje wanunue kwako.

Wafanye wateja wako sehemu ya wadau muhimu wa biashara yako ili wawe mabalozi wazuri huko nje.

Inabidi ukae kichwani kwa wateja,hata wakipata mtu huko nje wakufikirie wewe kwanza.

Hutapata wateja wanaokusema vizuri au wanaonunua kwako tena kama huna huduma nzuri na hutoi bidhaa au huduma zenye ubora pia.

Thaminisha huduma au bidhaa zako ili upunguze gharama ya kujitangaza kwa gharama kubwa kila wakati.

Mchumi Consulting 
0714260266
#biashara #masoko #matangazo #mtandaoni

MFANYABIASHARA JIUNGE BURE NA GROUP LETU LA WASAP KUPATA MASOMO NA UPDATES ZETU MUDA WOTE
👇👇👇

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA