UKIWA MGENI KWENYE BIASHARA USIKIMBILIE KUWINDA WATEJA FANYA HILI KWANZA
Imekua ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wapya kwenye biashara fulani kufikiria kupata mauzo mengi mwanzoni wakati wanaanza.
Wengi wanakua na matarajio makubwa ya kuuza na huvyo muda na nguvu nyingi wanatumia kusaka na kuwinda wateja.
Badala ya kutumia muda mwingi na nguvu katika kutengenenza thamani na kujenga jina la biashara yake kwanza.
Unakuta mfanyabiashara ni mpya kabisa kwenye biashara lakini anakua na matarajio makubwa au afanane idadi ya wateja na wenzie walio na miaka mitano kwenye biashara hiyo hiyo.
Mfano wewe unafanya biashara yako kwa kutangaza bidhaa au huduma zako mtandaoni na hapo ulipo una wafuasi(followers) elfu moja unataka ufanane na mwenzio alie na followers elfu 10.
Ukiwa na matarajio makubwa yatakufanya upaniki pale ambapo utakua hupati wateja.
Cha msingi cha kufanya kwanza inabidi ujenge jina ili ujulikane kwanza na vile vile ujifunze namna ya kujenga thamani ya huduma au bidhaa unayouza.
Ukiwa kama wale wafanyabiashara wanaopenda shortcut kwenye biashara utaishia kufeli na mwisho wa siku biashara itakufa.
Kumbuka biashara zinahitaji uvumilivu na maarifa,na pia kujipa muda ili biashara yako ikue nawe uwe unapata wateja wengi kama wenzio.
Jifunze mbinu zitakazo fanya uvutie wateja kwako ndani ya muda fulani.
Kuna mwingine ni mgeni kabisa katika biashara anajikuta analipia gharama kubwa kutangaza biashara yake, na matarajio yake ni kupata wateja wengi mwanzoni wakati anajua bado hana jina kubwa au hafahamiki kwenye soko husika.
Kumbuka wateja huwa wanapenda kununua bidhaa au huduma kwa watu wanaowafahamu na kuwaamini,hivyo nawe jenga jina ili uaminike kwanza.
Mchumi Consulting

Maoni
Chapisha Maoni