Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2026

MAKOSA 5 YANAYOFANYA BIASHARA IONGEZE MAUZO LAKINI IPOTEZE PESA

Picha
  Kuna tofauti kubwa kati ya biashara inayouza sana na biashara inayotengeneza pesa. Wakati mwingine unaweza kuona bidhaa zinatoka dukani kila siku, oda zinaongezeka, wateja wanaongezeka, na fedha nyingi zinaingia. Ukiangalia kwa haraka unaweza kusema: “Biashara hii inafanya vizuri sana!” Lakini si kila fedha inayoingia kwenye biashara ni faida. Unaweza kuongeza mauzo kutoka TZS 30 milioni hadi TZS 50 milioni, lakini mwisho wa mwezi ukawa na pesa kidogo kuliko ulivyokuwa na TZS 30 milioni. Kwa nini? Kwa sababu biashara haipotezi pesa kwa kukosa mauzo tu. Wakati mwingine inapoteza pesa kwa namna inavyofanya hayo mauzo. Haya ndiyo makosa 5 ambayo mfanyabiashara anapaswa kuyaangalia. 1. KUKIMBIZA MAUZO BILA KUANGALIA FAIDA (PROFIT) Mfanyabiashara anaweza kuweka lengo: “Mwezi huu lazima tufikishe TZS 100 milioni za mauzo.” Hilo ni jambo zuri. Lakini siyo mwisho wa hadithi. Jiulize pia: “Hizo TZS 100 milioni zimetuachia faida kiasi gani?” Mfano, biashara inaweza kuuza bidhaa za TZS 100...

MTEJA HAPIMI BEI PEKEE-FAHAMU TABIA ZA WATEJA

Picha
  Katika biashara kuna somo muhimu unalotakiwa kulifahamu kama mfanyabiashara ambalo ni “Consumer Behaviour Dynamics.” Ni somo linalokusaidia kuelewa kwa nini mteja ananunua. Kwa nini anachagua biashara moja na kuacha nyingine, kwa nini wakati mwingine anakataa bei fulani lakini anakubali kulipa bei kubwa sehemu nyingine, na kwa nini mteja anaweza kubaki mwaminifu kwenye biashara fulani hata kama kuna sehemu nyingine yenye bei ya chini. Ukiielewa vizuri tabia ya mteja, utaanza kuangalia biashara kwa macho tofauti. Utaacha kujiuliza tu, “Niuze kwa bei gani?” na utaanza kujiuliza, “Mteja anaona thamani gani kwenye kile ninachompa?” Na hapa ndipo wafanyabiashara wengi wanapokosea. Mfanyabiashara akiona mshindani wake anauza bidhaa kwa bei ya chini, jambo la kwanza analofikiria ni: “Basi na mimi nishushe bei.” Na hapo ndipo vita ya bei inaanza. Mmoja anauza 100,000. Mwingine anashusha mpaka 95,000. Mwingine anakuja na 90,000. Mwisho wa siku, kila mtu anashusha bei, lakini hakuna anayes...