Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2024
Picha
 MAMBO 8 YA KUFANYA ILI USITAPELIWE MTANDAONI Matapeli mtandaoni wameongeza spidi ya kutapeli watu. Nawe inabidi ujue namna ya kuchukua tahadhari ili usitapeliwe. 1.USIFANYE MALIPO HARAKA HARAKA Hata kama umeona bidhaa au huduma inakuvutia kwa mara ya kwanza hasa kwa mtu usiemfahamu usikimbilie kulipia haraka  Jipe muda huenda ni hisia zako za tamaa zinakufosi ulipie kwa sasa. Kumbuka matapeli wana lugha ya kuvutia sana. 2.KUWA MAKINI NA VITU AU HUDUMA ZA BEI NDOGO SANA Kuna wale watu wanatangaza wanauza vitu au huduma kwa BEI ndogo sana. Hadi unajiuliza anapataje faida? Kuwa makini matapeli huwa wanaweka vitu bei ndogo ili kukuvutia ili ukilipia tu basi humpati tena. 3.FANYA UTAFITI KUHUSU TAARIFA ZA MHUSIKA Kabla hujalipia bidhaa au huduma kwa mtu usiemfahamu ni vizuri kufanya utafiti kwanza. Angalia mawasiliano yake,anapatikana wapi, na vitu vingine vingi. Mara nyingi matapeli taarifa zao huwa zimejificha ficha hazieleweki,ukijaribu kumpigia simu au video call hapokei au h...
Picha
 JUA NAMNA TANO (5) YA KUUZA KWA KUTEKA HISIA ZA MTEJA Hivi umewahi nunua kitu wakati ukiwa na furaha sana halafu baadae ukajikuta unajutia maamuzi ya manunuzi yako? Au yale maamuzi ya kitu fulani ulinunua kwasababu ya uwoga tu uliokua nao kwa kuogopa labda kile kitu kitaisha,ukajikuta unanunua haraka haraka. Halafu siku zinaenda unakuta kile ulichonunua hakina manufaa au kinaendelea kuwepo lakini wewe uliogopa ukajua baadae huenda kitaisha dukani n.k Hizo ni baadhi ya hisia ambazo huwa zinawakuta watu na hujikuta wakifanya maamuzi kwa kuendeshwa na hisia badala ya fikra za kimantiki(logic).  Kuuza kwa kuzingatia hisia alizonazo mteja ni jambo la msingi kuliko hata huduma au bidhaa yako ilivyo. Kwani huwa inaaminika kuwa watu huwa wananunua vitu/huduma kutokana na hisia watakazopata kutoka kwenye hiyo huduma/bidhaa kuliko hata,namna bidhaa au huduma hiyo ilivyo.  Hii kwa maana nyingine ni kuwa watu huwa wananunua kutokana na namna watakavyojisikia wakiwa na kitu ulichowau...
Picha
  UMUHIMU WA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA BIASHARA YAKO Biashara nyingi huporomoka au nyingine hufa kabisa kutokana na kutokuwepo kwa mikakati bora ya ufuatiliaji mwenendo wa biashara husika.  Watu wengi hujikuta wamefanya matumizi makubwa mpaka wanajikuta wametumia na mtaji wa biashara. Hii husababishwa na uzembe wa kutotunza kumbukumbu au taarifa za mapato yanayoingia na matumizi. Biashara yoyote ili iweze kufanikiwa,utunzaji wa kumbukumbu ni nguzo muhimu sana. Kuna msemo huwa unasema “mali bila daftari huisha bila habari” NI KWANINI WATU HAWATUNZI KUMBUKUMBU ZA BIASHARA? Kuna sababu kadhaa ambazo huwa zinafanya watu waone shida kutunza kumbukumbu za biashara,tutaziangalia baadhi yake hapa chini. KUKOSA ELIMU YA KIBIASHARA Watu wengi huanzisha biashara kabla au pasipo kupata elimu ya kutosha kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia katika ufanyaji biashara. Na mojawapo ya elimu hizi ni pamoja na elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara.  Hivyo hujikuta wakipot...