
MAKOSA 10 UNAYOFANYA WAKATI WA KUUZA BIDHAA/HUDUMA YAKO NA NAMNA YA KUYAEPUKA Kuuza bidhaa au huduma ni sanaa ambayo lazima ufahamu kanuni zake. Ndio maana wewe na mwenzako mnaweza kuwa mnauza bidhaa au huduma inayofanana lakini mwenzio anauza zaidi ila wewe unaishia kuza kidogo. Kuna baadhi ya makosa ambayo wafanyabiashara wengi wamekua wakiyafanya mara kwa mara lakini hawajui kuwa ni makosa,na huwa yanafanya wasiuze au watumie nguvu kubwa kushawishi mteja. 1.KUTOMSIKILIZA MTEJA VIZURI Hii ni changamoto pale ambapo wewe muuzaji unakua muongeaji kupita kiasi na kutompa mteja nafasi ya kuongea au kuuliza maswali. Kimsingi wewe unatakiwa usiwe muongeaji sana zaidi ya mteja. Fanya Hivi Tumia muda mwingi kumsikiliza vizuri mteja ana changamoto gani au anahitaji huduma ipi,na wewe jikite kumuuliza maswali machache ili ufahamu shida yake zaidi. 2.KUFOKASI KWENYE MUONEKANO WA BIDHAA BADALA YA FAIDA ILIYOPO Hii imekua changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wengi ambapo wao huzingatia zaidi...