Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2024
Picha
MAKOSA 6 YATAKAYOFANYA AKAUNTI YAKO YA WASAP IFUNGWE  Haya ndio makosa 6 ukiyafanya yanaweza sababisha akaunti yako ya WhatsApp izuiwe au kufungwa kabisa kutumika. 1. KUTUMIA TOLEO LISILO RASMI LA WHATSAPP  Hapa ni kwa wewe unaependa kutumia App ambazo sio rasmi kwa ajili ya WhatsApp. Hapa tunamaanisha Apps kama WhatsApp GB au WhatsApp Plus,itafanya akaunti yako kufungwa. Kwani WhatsApp hawataki utumie toleo lisilo rasmi,hivyo achana na hizo WhatsApp GB na matoleo mengine ya hovyo. 2.KUTUMA VITISHO AU MAUDHUI MABAYA Kutuma ujumbe wa vitisho au kudhihaki wengine au kufanya watu wawe na hofu. Ukifanya matendo haya kwa muda mrefu utakuja kukuta akaunti yako ya WhatsApp imezuiwa kufanya kazi,hivyo kuwa makini na ujumbe wa kutishia watu. 3.UKIRIPOTIWA MARA KWA MARA NA WATU Kama endapo utakuwa unaripotiwa mara nyingi na watu basi jua muda sio mrefu akaunti yako itafungwa. Hivyo tumia WhatsApp kiustaarabu na kiusalama ili watu wasitume report kuwa unawakera. 4.KUUNGA WATU KWENYE MAGR...
Picha
  SABABU 9 ZA KUZUIWA AKAUNTI YA KURUSHA TANGAZO LAKO KUKATALIWA MTANDAONI(FACEBOOK/INSTAGRAM) Mitandao ya kijamii imekua msaada mkubwa sana wa kuzikutanisha biashara na wateja mbalimbali hivi sasa. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii imekua maarufu sana siku hizi kwa ajili ya wafanyabiashara kutangaza bidhaa au huduma zao. Mitandao ya kijamii kama Instagram,Facebook,Tweeter na mingineyo imekua njia mojawapo ya pendwa sana ya kufanyia biashara.  Uzuri wa kutangaza biashara kupitia mitandao ya kijamii ni kuwa unakutana na watu wengi(audience) kwa gharama ndogo sana. Sasa ili uweze kufanya matangazo ya kulipia mitandaoni kama Facebook au Instagram utapaswa uwe na akaunti maalumu zilizo katika sifa ya kufanyia biashara(business account).  Na uzuri ni kwamba hata akauti yako ya kawaida ya Facebook au Instagram au tweeter unaweza ukaifanya ikawa na uwezo wa kufanya matangazo ya kulipia(business account) Unaweza pia ukafanya matangazo ya kulipia kupitia google au youtube ambapo ...
Picha
  NINI MAANA NA FAIDA YA KUIFANYA BIASHARA YAKO KUWA KAMPUNI Kampuni ni chombo cha kisheria  kinachoundwa na watu wawili au zaidi kwa nia ya kuendesha biashara au shuguhuli nyingine yoyote ya kiuchumi au kijamii. Kwa Tanzania mamlaka inayosimamia usajili wa makampuni ni BRELA chini ya sheria ya Makampuni ya mwaka 2002. Kampuni ina uwepo wa kisheria  tofauti na wamiliki au wanahisa wa kampuni husika. Vilevile Kampuni inaweza kumiliki mali,kuingia mikataba,kushitaki au kushitakiwa na kulipa kodi kwa kutumia jina lake. Kuna faida nyingi sana ambazo zinapatikana kama endapo utaamua kuifanya biashara yako iwe katika mfumo wa kampuni tofauti na ikiwa katika mfumo wa kawaida wa jina la biashara. Na katika andiko letu tutaelezea baadhi ya faida zinazopatikana ambazo utazipata tu pale ukiisajili biashara yako katika mfumo wa kampuni. 1.Faida upande wa kodi(Tax benefits) Miongoni mwa faida unayopata ukiwa umesajili biashara katika mfumo wa kamapuni ni upande wa kodi unayolipa. Mara...