AINA TATU(3) ZA WATU(NETWORKS) UNAOTAKIWA KUWA NAO
Kutengenenza na kuendeleza aina tofauti ya mtandao wa watu(networks) ni jambo la muhimu sana kwa ajili ya maendeleo yako binafsi au kwenye career yako fulani ambayo upo nayo.
Tumeelezea aina 3 (tatu) muhimu za mtandao wa watu(networks) ambao unatakiwa usikose ili uweze kufanikiwa katika Maisha kwa ujumla.
1. MTANDAO WA WATU WAKO BINAFSI(Personal Networks)
Hii ni network muhimu ambayo hutakiwi kukosa. Hawa ni watu wako wa karibu sana ambao cha kwako ni chao,na chao ni chako.
-Hawa ni watu wa karibu kama vile familia yako,ndugu mnaoelewana,na marafiki wa karibu amabo sio wanafiki.
-Hawa watu wapo tayari kusimama na wewe kwenye shida na raha.
-Hawa ndio kimbilio lako la haraka pale unahitaji msaada au ushauri flani.
-Hawa ni wale watu ambao wapo tayari kutunza siri zako na una waamini.
-Hawa ndio watakaokusaidia pindi unaumwa na pia watakuzika.
-Hawa ndio wanaokusemea vizuri sehemu(refferals) na pia wanakupa fursa mbalimbali za kimaisha.
-Hawa ndio wafariji wako.
Hakikisha hukosi watu hawa katika Maisha yako,je wewe unao watu hawa?
2.MTANDAO WA WATU WAKO WA KIKAZI(Operational Networks)
Hii nayo ni network ya muhimu sana kuwa nayo ili uweze kufanikiwa kwenye malengo yako.
Hawa ni watu wako ambao unakua nao kikazi,au biashara au kwenye taaluma yako flani ambayo upo nayo.
Hawa ndio watu wanaokusaidia mambo yako ya kikazi au biashara yaweze kwenda bila wewe kutumia nguvu kubwa.
Mfano wewe ni mfanyabiashara utahitaji mtu wa kukupa connection na fursa mpya za biashara na mambo mengine mengi.
Kiufupi huu ni mtandao wa watu ambao wanafanya mambo yako ya kila siku yaweze kwenda.
Hawa anaweza kuwa ni derava wako,fundi wako,bodaboda wako,dalali wako n.k
Unaweza usione umuhimu wa watu hawa mpaka upate changamoto.
Kumbuka sio kila kitu utahitajika kufanya au kuwepo wewe mwenyewe moja kwa moja hivyo utahitaji watu wa haraka wa kufanya au kutatua changamoto zako.
Hakikisha hukosi kuwa na watu hawa kwenye Maisha yako. Je wewe unao watu hawa?
3.MTANDAO WA WATU WA KIMIKAKATI(Strategic Networks)
Hawa ni watu muhimu ambao ni nje ya control yako ya moja kwa moja lakini una uhusiano nao katika hali flani.
Watu hawa anaweza kuwa ni kiongozi mwandamizi wa eneo fulani,au mtaalamu wa taasisi fulani,au mtu yeyote mwenye ushawishi(influence).
Huyu anaweza kuongea jambo fulani sehemu kuhusu wewe na ukajikuta umepata fursa ambayo usingeipata kama usingefahamiana nae.
Kuna watu wanapata deals na tenda sehemu kwasababu tu anafahamiana na mkubwa wa taasisi husika.
Kuna watu hawapati kashikashi fulani fulani kwasababu anafahamiana na mkubwa fulani.
Watu hawa anaweza kuwa mwanasheria,meneja sehemu,polisi,mtu maarufu,Daktari,kiongozi wa dini n.k
Aisee hakikisha hukosi mtu wa namna hii,itafanya mambo yako yawe mepesi.
Je wewe unao mtandao wa watu kama hawa?
MWISHO
Anza sasa kujenga mahusiano mazuri na watu,na hakikisha mahusiano yako yanakua ya watu ambao utanufaika nao katika hali moja au nyingine.
Ishi na watu vizuri,be humble.
IMEANDIKWA NA
Mchumi Consulting
0714260266
JIUNGE BURE KWENYE GROUP LETU LA WASAP LA BIASHARA NA MASOKO MTANDAONI HAPA CHINI👇👇

Maoni
Chapisha Maoni