Ajira na Biashara: Kwanini Nidhamu ndio Tofauti ya Kufanikiwa na Kufeli



Watu wengi wanaingia kwenye ujasiriamali wakiamini kuwa wanatafuta "uhuru." Uhuru wa kutokuwa na bosi, uhuru wa kuamka muda wanaotaka, na uhuru wa kufanya mambo yao wenyewe.


Lakini ukweli mchungu ni kwamba, biashara ni bosi mkali kuliko bosi yeyote uliyewahi kukutana naye ofisini.


Tazama picha halisi kuhusu dhana hii,Leo, tuchambue kwa kina kwanini biashara inahitaji nidhamu kubwa na jinsi unavyoweza kuitumia ajira yako kama darasa la mafanikio.


1. Kwenye Biashara, "Kutegea" Ni Sawa na Kufilisika

Kwenye ajira, unaweza kuwa na siku ambayo huna mzuka wa kazi lakini mshahara wako ukabaki palepale mwisho wa mwezi. Lakini kwenye biashara, ukilala na biashara inalala. Biashara haina "sikukuu" wala "leave" ya kulipwa kama wewe ndiye injini ya kila kitu.


Kila sekunde unayopoteza, ni mteja anayepotea au gharama zinazoongezeka. Hapa ndipo nidhamu inapohitajika—uwezo wa kufanya kazi hata wakati ambao hujisikii kufanya hivyo.


2. Stress za Biashara vs Stress za Ajira

Watu wengi wanalalamika kuhusu stress za ofisini, lakini stress za biashara ziko "level" nyingine.


  Kwenye Ajira: Stress inaweza kuwa ni kutokuelewana na bosi au wingi wa kazi.

 Kwenye Biashara: Stress ni kujiuliza utalipaje kodi ya pango, utawalipaje wafanyakazi, na utafanya nini kama mzigo haujatoka bandarini au wateja hawanunui.


Kujisimamia mwenyewe kunahitaji uwe na akili ya chuma (mental toughness) kwa sababu hakuna mtu wa kukusukuma isipokuwa malengo yako.


3. Ajira Kama Darasa la Bure

Kosa kubwa wanalofanya wafanyakazi wengi ni kudharau kazi zao za sasa. Hii inatukumbusha kuwa: Ajira inatakiwa iwe darasa.


Unapofanya kazi kwa mtu mwingine, unajifunza vitu vingi kwa gharama za huyo bosi:

 Mifumo ya Usimamizi: Jinsi kampuni inavyopanga bajeti na kusimamia watu.

 Huduma kwa Wateja: Jinsi ya kudeal na wateja wagumu.

 Nidhamu ya Muda: Kufika kazini saa mbili asubuhi kila siku kunakujengea misuli ya nidhamu utakayoihitaji kwenye biashara yako.


Hitimisho

Kabla hujaacha kazi na kukimbilia kwenye biashara, jiulize: Je, nina nidhamu ya kutosha kujisimamia bila kusimamiwa? Kama huwezi kuwa mfanyakazi bora unaposimamiwa na wengine, itakuwa vigumu sana kuwa bosi bora unayejisimamia mwenyewe.


Tumia muda wako wa ajira kujifunza, jenga nidhamu, na uelewe kuwa biashara ni marathon, sio mbio za mita mia.


Paul Chengula

0714 260266


TAZAMA HUDUMA ZETU HAPA


Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KUWA NA KAMPUNI NA NAMNA YA KUGAWA HISA NA KUISAJILI HAPA TANZANIA

MFAHAMU PAUL CHENGULA

KITABU CHA MISINGI YA UWEKEZAJI:FAHAMU SIRI ZA KUANZA KUWEKEZA KWENYE HISA NA BOND NA JINSI YA KUEPUKA HASARA