MTEJA HAPIMI BEI PEKEE-FAHAMU TABIA ZA WATEJA

 


Katika biashara kuna somo muhimu unalotakiwa kulifahamu kama mfanyabiashara ambalo ni “Consumer Behaviour Dynamics.”

Ni somo linalokusaidia kuelewa kwa nini mteja ananunua.

Kwa nini anachagua biashara moja na kuacha nyingine, kwa nini wakati mwingine anakataa bei fulani lakini anakubali kulipa bei kubwa sehemu nyingine, na kwa nini mteja anaweza kubaki mwaminifu kwenye biashara fulani hata kama kuna sehemu nyingine yenye bei ya chini.

Ukiielewa vizuri tabia ya mteja, utaanza kuangalia biashara kwa macho tofauti.
Utaacha kujiuliza tu, “Niuze kwa bei gani?” na utaanza kujiuliza, “Mteja anaona thamani gani kwenye kile ninachompa?”
Na hapa ndipo wafanyabiashara wengi wanapokosea.

Mfanyabiashara akiona mshindani wake anauza bidhaa kwa bei ya chini, jambo la kwanza analofikiria ni:

“Basi na mimi nishushe bei.”
Na hapo ndipo vita ya bei inaanza.
Mmoja anauza 100,000.
Mwingine anashusha mpaka 95,000.
Mwingine anakuja na 90,000.

Mwisho wa siku, kila mtu anashusha bei, lakini hakuna anayesimama kujiuliza:
“Mteja anachagua biashara kwa sababu ya bei tu?”
Jibu ni hapana.

Bei ni muhimu, lakini siyo kitu pekee ambacho mteja anaangalia.
Mteja anaangalia pia thamani anayopata kwa kile anacholipa.

Hii ndiyo tunaita Perceived Value — kwa lugha rahisi, ni thamani ambayo mteja anaiona na kuihisi kutokana na bidhaa au huduma yako.
Na hapa ndipo mambo yanakuwa interesting.

Fikiria kuna biashara mbili
Tuseme kuna Biashara A na Biashara B.
Biashara A inauza bidhaa kwa:
TZS 100,000
Biashara B inauza bidhaa hiyo hiyo kwa:
TZS 130,000
Kwa kuangalia bei tu, utaona Biashara A ndiyo imeshinda.
Lakini hebu tuangalie upande wa mteja.

Biashara A:
Mteja anasubiri muda mrefu.
Hakuna delivery.
Huduma siyo nzuri sana.
Akipata tatizo baada ya kununua, anapata msaada kwa shida.
Mahali pa biashara siyo rahisi kufika.
Mteja hana uhakika sana na quality.

Biashara B:
Anapata huduma haraka.
Bidhaa inaletwa kwake.
Anaelezewa vizuri kabla ya kununua.
Kuna warranty au support baada ya mauzo.
Malipo ni rahisi.
Anajua akipata tatizo kuna mtu wa kumsaidia.
Anaamini quality ya bidhaa.
Sasa mteja anaweza kusema:

“Ni kweli Biashara A ni rahisi kwa TZS 30,000, lakini Biashara B inanipa vitu ambavyo ni muhimu kwangu.”
Na akaenda Biashara B.
Je, amekosea?

Siyo lazima.
Kwa sababu yeye hakuwa anaangalia TZS 100,000 dhidi ya TZS 130,000 pekee.
Alikuwa anaangalia:
“Kwa hela ninayolipa, ninapata nini?”
Hapo ndipo Perceived Value inapokuja.

MTEJA HAANGALII FEDHA PEKEE
Wakati mwingine sisi wafanyabiashara tunafikiria kwamba gharama ya mteja ni hela anayolipa.
Lakini si hivyo.
Mteja anaweza pia kuangalia:
⏱️ Muda — Nitamaliza huduma kwa muda gani?
๐Ÿ˜“ Usumbufu — Nitatakiwa kufuatilia mara ngapi?
⚠️ Risk — Nikilipa, nina uhakika nitapata nilichoahidiwa?
๐Ÿค Huduma — Watanihudumiaje?
๐Ÿšš Urahisi — Bidhaa itanifikia kwa urahisi?
๐Ÿ”„ Baada ya mauzo — Nikiona tatizo, watanisaidia?
๐Ÿ” Uaminifu — Ninaweza kuwaamini?
Kwa hiyo, mteja anaweza kuona bidhaa ya TZS 130,000 ni “nafuu” kwake kuliko bidhaa ya TZS 100,000.
Kwa nini?

Kwa sababu ile ya TZS 100,000 inaweza kumgharimu zaidi kwenye muda, usumbufu, risk na stress.

MFANO MWINGINE: MIGAHWA MIWILI
Hebu fikiria kuna migahawa miwili.

Mgahawa A
Chakula ni TZS 10,000.
Lakini ukifika:
Unasubiri dakika 40.
Mhudumu anachelewa.
Wakati mwingine chakula kiko vizuri, wakati mwingine hakiko vizuri.
Parking ni shida.
Na ukipata tatizo, hakuna anayejali sana.

Mgahawa B
Chakula ni TZS 18,000.
Lakini:
Unaagiza haraka.
Chakula kinatoka kwa muda mzuri.
Quality iko consistent.
Wahudumu wanajua kazi.
Mazingira ni mazuri.
Malipo ni rahisi.
Na ukihitaji msaada, unapata.
Sasa kuna mtu anaweza kusema:
“Kwa nini nilipie 18,000 wakati kuna sehemu ya 10,000?”
Lakini mwingine anaweza kusema:

“Mimi bora nilipie 18,000. Sitaki kupoteza muda wangu na usumbufu.”
Hapo ndipo tunapoona kwamba:
Bei ya chini siyo kila wakati maana yake ni value kubwa.

Na pia:
Bei kubwa siyo kila wakati maana yake ni bidhaa ghali.
Kama mteja anaona anapata thamani inayostahili hela yake, anaweza kulipa.

PERCEIVED VALUE NI NINI HASA?
Kwa lugha rahisi sana:

Perceived Value ni namna mteja anavyoona thamani ya kile unachompa ukilinganisha na kile anachotoa.
Anaweza kutoa:
Pesa
Muda
Juhudi
Uvumilivu
Risk
Stress
Na anatarajia kupata:
Ubora
Urahisi
Usalama
Huduma nzuri
Matokeo mazuri
Comfort
Confidence
Experience nzuri

Kwa hiyo, kama unataka mteja aone biashara yako ina value, usifikirie tu:
“Tunauza kwa bei gani?”
Anza kufikiria:
“Mteja anapata nini kwa hiyo bei?”

HAPA NDIPO BIASHARA NYINGI ZINAKOSEA
Mfanyabiashara anaweza kusema:
“Bidhaa yangu ni nzuri.”
Sawa.

Lakini mteja anaiona?
Anaelewa kwa nini ni nzuri?
Anaona tofauti yake na bidhaa nyingine?
Anaamini hiyo quality?
Au wewe ndiye unayejua tu kwamba bidhaa yako ni nzuri?
Hili ni jambo muhimu sana.

Value ambayo mteja haioni, haielewi au haiamini, ni vigumu kwake kuithamini.

Kwa hiyo kama una:
Delivery nzuri — mwambie.
Warranty nzuri — mweleze.
After-sales service — ionyeshe.
Quality nzuri — thibitisha.
Huduma ya haraka — mteja aipate kweli.
Urahisi wa malipo — mweleze.
Uaminifu — ujenge kupitia matendo.
Usifikiri mteja ataona kila kitu mwenyewe.

Wakati mwingine unatakiwa kumsaidia aone value uliyonayo.

KWA NINI MTU ANALIPA ZAIDI?
Hili ni swali ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kujiuliza.

Kwa nini mtu anunue kwangu kwa TZS 150,000 wakati mwingine anauza TZS 120,000?

Kama jibu lako ni:
“Kwa sababu bidhaa yangu ni nzuri.”
Haitoshi.

Jiulize zaidi:
Je, ninampa huduma bora?
Je, ninaokoa muda wake?
Je, ninapunguza risk yake?
Je, ninampa convenience?
Je, anaweza kuniamini?
Je, nikishauza nitakuwa bado niko naye?
Je, experience yake ni nzuri?
Je, bidhaa yangu inampa matokeo bora?
Hizo ndizo sababu zinazoweza kumfanya mteja akubali kulipa zaidi.

USISHINDANE KWA BEI PEKEE
Kuna tofauti kati ya kusema:

“Sisi ni cheap.”
na kusema:
“Sisi tuna value.”
Ukijenga biashara yako kwa bei ya chini pekee, siku mshindani wako akishusha bei zaidi unaweza kuanza kupoteza wateja.

Lakini kama umejenga biashara ambayo mteja anaiona ina:
Ubora + Uaminifu + Urahisi + Huduma + Experience + Matokeo
mshindani wako akishusha bei kidogo siyo lazima mteja akimbie.
Kwa sababu tayari ana sababu nyingine za kukuchagua.

SWALI LA MUHIMU KWA MFANYABIASHARA
Leo usijiulize tu:
“Bei yetu iko chini kuliko ya mshindani?”
Jiulize:
“Mteja anapata value gani zaidi akija kwetu?”
Na swali lingine ambalo ni muhimu zaidi:

“Kama kesho mshindani wangu atashusha bei kuliko mimi, ni kitu gani kitamfanya mteja wangu bado abaki kwangu?”

Kama una jibu zuri la swali hili, kuna uwezekano mkubwa kwamba una kitu muhimu zaidi ya bei:

UNA THAMANI AMBAYO MTEJA ANAIONA.
Mwisho wa siku, biashara siyo kuhusu nani anauza kwa bei ya chini zaidi.

Ni kuhusu nani anaweza kumpa mteja thamani anayohisi inastahili kile anacholipa.
Mteja haangalii tu bei iliyo kwenye tag. Anaangalia experience nzima.

Na wakati mwingine, TZS 150,000 yenye value inaweza kuonekana nafuu kuliko TZS 100,000 yenye usumbufu.

IMEANDIKWA NA
Paul Chengula
+255 714 260266

Jiunge na channell yetu ya wasap hapo chini kwenye link๐Ÿ‘‡
https://whatsapp.com/channel/0029Va8wXM54dTnFbkbyUv2f

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUWEKEZA NA KUMILIKI HISA ZA MAKAMPUNI YA TANZANIA

KITABU CHA MISINGI YA UWEKEZAJI:FAHAMU SIRI ZA KUANZA KUWEKEZA KWENYE HISA NA BOND NA JINSI YA KUEPUKA HASARA

MFAHAMU PAUL CHENGULA