MAKOSA 5 YANAYOFANYA BIASHARA IONGEZE MAUZO LAKINI IPOTEZE PESA
Kuna tofauti kubwa kati ya biashara inayouza sana na biashara inayotengeneza pesa. Wakati mwingine unaweza kuona bidhaa zinatoka dukani kila siku, oda zinaongezeka, wateja wanaongezeka, na fedha nyingi zinaingia. Ukiangalia kwa haraka unaweza kusema: “Biashara hii inafanya vizuri sana!” Lakini si kila fedha inayoingia kwenye biashara ni faida. Unaweza kuongeza mauzo kutoka TZS 30 milioni hadi TZS 50 milioni, lakini mwisho wa mwezi ukawa na pesa kidogo kuliko ulivyokuwa na TZS 30 milioni. Kwa nini? Kwa sababu biashara haipotezi pesa kwa kukosa mauzo tu. Wakati mwingine inapoteza pesa kwa namna inavyofanya hayo mauzo. Haya ndiyo makosa 5 ambayo mfanyabiashara anapaswa kuyaangalia. 1. KUKIMBIZA MAUZO BILA KUANGALIA FAIDA (PROFIT) Mfanyabiashara anaweza kuweka lengo: “Mwezi huu lazima tufikishe TZS 100 milioni za mauzo.” Hilo ni jambo zuri. Lakini siyo mwisho wa hadithi. Jiulize pia: “Hizo TZS 100 milioni zimetuachia faida kiasi gani?” Mfano, biashara inaweza kuuza bidhaa za TZS 100...