Machapisho

Picha
FAHAMU BIASHARA 19 ZA KUANZA NA MTAJI MDOGO ZENYE FAIDA Tuangalie biashara 19 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000(laki moja) unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa. Hakuna biashara ndogo, ila kuna biashara unazoweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa. Hiyo ambayo inaitwa “biashara ndogo” ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku itakutoa. Kabla hatujaenda kwenye hiyo orodha ya hizo biashara za mtaji mdogo, hebu tuweke sawa kauli ya “zenye faida kubwa”. Faida kubwa haimaanishi mamilioni ya fedha, bali ni kwamba faida utakayoipata kulingana na mtaji wako ni nzuri na usipokata tamaa itakufikisha mbali. ZINGATIA: Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile, ni vyema kufuatilia utaratibu na sheria za mahali ulipo. Tafadhali ilinde biashara yako kwa kufuata kanuni zote zilizowekwa na serikali. Baada ya kulisawazisha hilo, twende kwenye hiyo orodha ya biashara za mtaji md...
Picha
ZINGATIA HATUA HIZI 6 ILI UFIKIE UHURU WAKO WA  KIFEDHA KIURAHISI Kila mmoja huwa ana ndoto fulani ya kuwa siku moja awe na pesa nyingi ili aweze kutimiza mahitaji mbalimbali. Lakini huwezi kufikia uhuru huo wa kifedha kama endapo hutachukua hatua kadhaa sasa. Tumeelezea baadhi ya hatua sita(6) ambazo ukizichukua zitakufanya uepukane na suala la kuhangaika na uhaba wa kifedha mara kwa mara. 1. FUTA MADENI YENYE RIBA KUBWA Moja ya kitu kinachomaliza pesa zako ni madeni yenye riba kubwa.  Ni kweli mkopo sio mbaya lakini pale ambapo unachukua mikopo yenye riba kubwa sana huwa inaumiza. Kumbuka riba ni gharama ya mkopo uliochukua,lakini kama endapo utakua na mikopo mingi yenye riba kubwa jua kiasi kikubwa cha pesa utakua unatumia kulipa riba za mikopo, na kuwafaidisha waliokupa mkopo,hivyo kuwa makini kwenye hili. 2.PUNGUZA MATUMIZI YASIYO NA ULAZIMA Anza sasa kujifanyia tathimini juu ya matumizi yako kwenye vitu unavyopenda kununua. Jilulize je hiki kitu kina umuhimu kwa sasa,au ...
Picha
 FAHAMU MAKOSA 8 WANAYOFANYA WAUZAJI WAKATI WA KUUZA BIDHAA/HUDUMA ZAO Kufanya mauzo ni sanaa tunasema “sale is art”,maana yake ni inahitaji kipaji na ujuzi ili kuwa muuzaji mzuri.  Kama ilivyo kwenye mchezo wowote,ili kupata mafanikio ni muhimu,kufanya mazoezi,kufanya makosa,na kujifunza zaidi na pia kutokata tamaa pale unaposhindwa kupata matokeo uliyokuwa unayategemea. Hapa tutazungumzia makosa kadhaa ambayo wauzaji(sales person) wengi huyafanya pale wanapotaka kuuza bidhaa au huduma waliyo nayo kwa mteja mpya.  Yawezekana unafahamu baadhi ya step muhimu wakati wa kuuza bidhaa au huduma yako kwa mara ya kwanza hasa kwa mteja mpya,asie kufahamu na huenda haifahamu bidhaa yako pia. Kuna aina fulani ya makosa ambayo wengi wamekua wakiyafanya wakati wa kushawishi kuuza huenda ni bidhaa au huduma fulani. 1. KUONGEA SANA NA KUTOSIKILIZA Ni muhimu kuongea wakati wa kufanya mauzo na kushawishi mauzo ya bidhaa au huduma yako,lakini kuongea sana wewe peke yako kama muuzaji huwa ...
Picha
YAFAHAMU MAMBO 5 (MATANO) ILI KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO Dunia ya biashara imekua ikibadilika mara kwa mara,hii ikiwa ni pamoja na ujuzi au mikakati mbalimbali ambayo imekua ikitumika kulingana na aina ya biashara husika nayo huwa inabadilika. Haijalishi kama ndio unaanza biashara au ni mzoefu kwenye biashara fulani itakulazimu kuendana tu na mabadiliko mbalimbali ili uweze kufanikiwa kibiashara.  Katika andiko hili tutashirikishana mambo kama matano muhimu ili kusaidia kufanya biashara yenye mafanikio ili uweze kutimiza malengo yako uliyojiwekea. 1. JENGA JINA(BUILD A BRAND) Brand ni zaidi ya nembo ya biashara yako.  Huu ni utambulisho wa biashara yako na kwa namna gani unafikisha utambulisho huo kwa wateja wako. Ukiwa na brand(jina) kubwa ni rahisi kuwa mbele ya washindani wako,na vilevile utavutia watu wengine waje kwako na pia utaongeza thamani yako sokoni.   Hivyo ni muhimu sana ukaweka mikakati ya kujenga brand yako kwa kujitofutisha na washindani wako kwa k...