
MAMBO HAYA 5 YANAMALIZA FEDHA ZAKO Hivi umewahi jiuliza ni kwanini mtu fulani anapokea kipato kikubwa sana kama ni kazini au ofisi fulani au ana biashara ina mauzo makubwa sana,lakini mtu huyo kila siku anahangaika na madeni,au shida za pesa za hapa na pale. Kumbuka pesa huwa inahitaji nidhamu na huwa inahitaji heshima,kwa maana ya kwamba ukiiheshimu na kuwa na nidhamu nayo huwa inakaa kwako. Lakini ukii-treat vibaya nayo huwa inaondoka inakwenda kwa yule anaeipa heshima na kui-treat vizuri Kuna baadhi ya mambo ukiyaendekeza au ukiwa unayafanya mara nyingi inakua ni mara chache sana kubakia na pesa,na utajikuta kila siku unatafuta mchawi ni nani anaesababisha usifikie malengo fulani kwenye maisha yako. Leo tumeorodhesha mambo matano yanayotafuna pesa zako kimya kimya na wewe umekua ukiyachukulia kawaida 1. Matumizi kwenye vitu visivyo na ulazima Hili limekua ni eneo linalotafuna pesa za watu wengi sana,pale ambapo mtu unajikuta unaingia kwenye matumizi ya kununua vitu ambav...