MAMBO SABA (7) YA KUZINGATIA KABLA HUJAANZISHA BIASHARA MPYA Kuanzisha biashara ni uamuzi mkubwa na mzuri ambao huwa unahitaji kujiandaa na kuwa na mpango makini. Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla hujaanzisha biashara mpya ambayo yanaweza kufanya biashara yako ikafanikiwa au ikafa ambayo ni muhimu kuyafahamu Katika andiko hili tutangalia mambo kadhaa ya kuzingatia kabla hujafanya maamuzi hayo na ni kwa namna gani yatakusaidia ufikie malengo yako. 1. WAZO LA BIASHARA YAKO Jambo la kwanza na la muhimu la kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara mpya ni wazo la biashara unayotaka kuanzisha. Wazo la biashara ndio msingi wa biashara yako kwani unatakiwa uwe na wazo la biashara linaloeleweka vizuri. Wazo lako la biashara ni muhimu lijibu maswali haya: Bidhaa au huduma utakayotoa ni ipi? Kwa namna gani bidhaa yako itatatua changamoto za watu au kukidhi mahitaji yao? Ni kwa namna gani huduma yako itatofautiana na ya wenzako? Wazo lako la biashara ni muhimu pia likatokana na ...