MIKAKATI 6 YA KUFANYA ILI KUONGEZA MAUZO YA BIDHAA AU HUDUMA UNAYOUZA Mauzo mengi ni miongoni mwa malengo makuu na ya msingi kwa kila biashara. Hapa ina maana pale unapopata mauzo makubwa vilevile,utapata faida kubwa kwenye biashara husika. Sasa ni namna gani unaweza kufikia malengo ya kuwa na mauzo makubwa kwenye kile unachokiuza katika zama za ushindani mkubwa wa soko? Inatakiwa ujue mikakati na mbinu kadhaa za kukuwezesha kuuza zaidi na hivyo kuongeza faida zaidi. Katika blog post hii tutaelezea njia na mbinu kadhaa ambazo huwa zinaleta matokeo makubwa hasa pale unapotaka kuongeza mauzo zaidi. 1. UZA BIDHAA/HUDUMA YA NYONGEZA (Cross sell) Unaweza kutumia mbinu au mkakati huu pale unapotaka kuongeza mauzo zaidi kwa kumuuzia mteja bidhaa ya nyongeza inayoendana na bidhaa au huduma aliyokwisha kununua au aliyo na mpango wa kununua. Hapa unatakiwa ugundue hitaji la mteja juu ya bidhaa au huduma anayotaka na kumshauri achukue na bidhaa nyingine inayoendana na bidhaa anayotaka. Mfan...