Machapisho

Picha
  MIKAKATI 6 YA KUFANYA ILI KUONGEZA MAUZO YA BIDHAA AU HUDUMA UNAYOUZA Mauzo mengi ni miongoni mwa malengo makuu na ya msingi kwa kila biashara. Hapa ina maana pale unapopata mauzo makubwa vilevile,utapata faida kubwa kwenye biashara husika. Sasa ni namna gani unaweza kufikia malengo ya kuwa na mauzo makubwa kwenye kile unachokiuza katika zama za ushindani mkubwa wa soko? Inatakiwa ujue mikakati na mbinu kadhaa za kukuwezesha kuuza zaidi na hivyo kuongeza faida zaidi. Katika blog post hii tutaelezea njia na mbinu kadhaa ambazo huwa zinaleta matokeo makubwa hasa pale unapotaka kuongeza mauzo zaidi. 1. UZA BIDHAA/HUDUMA YA NYONGEZA (Cross sell) Unaweza kutumia mbinu au mkakati huu pale unapotaka kuongeza mauzo zaidi kwa kumuuzia mteja bidhaa ya nyongeza inayoendana na bidhaa au huduma aliyokwisha kununua au aliyo na mpango wa kununua. Hapa unatakiwa ugundue hitaji la mteja juu ya bidhaa au huduma anayotaka na kumshauri achukue na bidhaa nyingine inayoendana na bidhaa anayotaka. Mfan...
Picha
  MAMBO 5 ILI KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO Dunia ya biashara imekua ikibadilika mara kwa mara,hii ikiwa ni pamoja na ujuzi au mikakati mbalimbali ambayo imekua ikitumika kulingana na aina ya biashara husika nayo huwa inabadilika. Haijalishi kama ndio unaanza biashara au ni mzoefu kwenye biashara fulani itakulazimu kuendana tu na mabadiliko mbalimbali ili uweze kufanikiwa kibiashara.  Katika andiko hili tutashirikishana mambo kama matano muhimu ili kusaidia kufanya biashara yenye mafanikio ili uweze kutimiza malengo yako uliyojiwekea. 1. JENGA JINA(BUILD A BRAND) Brand ni zaidi ya nembo ya biashara yako. Huu ni utambulisho wa biashara yako na kwa namna gani unafikisha utambulisho huo kwa wateja wako. Ukiwa na brand(jina) kubwa ni rahisi kuwa mbele ya washindani wako,na vilevile utavutia watu wengine waje kwako na pia utaongeza thamani yako sokoni.  Hivyo ni muhimu sana ukaweka mikakati ya kujenga brand yako kwa kujitofutisha na washindani wako kwa kuwapa wateja bidha...
Picha
AINA TATU(3) ZA WATU(NETWORKS) UNAOTAKIWA KUWA NAO Kutengenenza na kuendeleza aina tofauti ya mtandao wa watu(networks) ni jambo la muhimu sana kwa ajili ya maendeleo yako binafsi au kwenye career yako fulani ambayo upo nayo. Tumeelezea aina 3 (tatu) muhimu za mtandao wa watu(networks) ambao unatakiwa usikose ili uweze kufanikiwa katika Maisha kwa ujumla. 1. MTANDAO WA WATU WAKO BINAFSI(Personal Networks) Hii ni network muhimu ambayo hutakiwi kukosa. Hawa ni watu wako wa karibu sana ambao cha kwako ni chao,na chao ni chako. -Hawa ni watu wa karibu kama vile familia yako,ndugu mnaoelewana,na marafiki wa karibu amabo sio wanafiki. -Hawa watu wapo tayari kusimama na wewe kwenye shida na raha.  -Hawa ndio kimbilio lako la haraka pale unahitaji msaada au ushauri flani. -Hawa ni wale watu ambao wapo tayari kutunza siri zako na una waamini. -Hawa ndio watakaokusaidia pindi unaumwa na pia watakuzika. -Hawa ndio wanaokusemea vizuri sehemu(refferals) na pia wanakupa fursa mbalimbali za kimai...
Picha
PROMOTE BIASHARA YAKO SASA KWENYE MTANDAO WA X (TWITTER) Mtandao wa X(zamani Tweeter) umekua ni mtandao unaotumiwa na watu wengi kwa sasa. Kuanza kufikiria namna ya kupromote biashara yako kwa kupitia matangazo ya kulipia kwenye mtandao huu ni jambo la muhimu. Kama ilivyo mitandao mingine kama vile Instagram,Facebook,Tikok na mtandao wa X nao unazo huduma za kupromote matangazo ya biashara yako. Kwa kuweka utaratibu mzuri wa kibajeti na kuwa na malengo yako ya kibiashara ni rahisi zaidi kuwafikia mamilioni ya watu waliopo kwenye mtandao wa X. VIGEZO VYAKE NI VIPI? Ili uweze kufanya matangazo ya kulipia katika mtandao wa X ni lazima uwe na akaunti ya mtandao wa X ambayo umeifanya kuwa ni ya biashara(professional account). Akaunti ya biashara inapatikana kwa kuibadilisha akaunti yako hiyo ya kawaida na kuipeleka iwe ya biashara kwa process ndogo kwenye App hiyo hiyo. Kuifanya akaunti kuwa ya biashara(professional account) ni sharti la muhimu kama ilivyo katika mitandao mingine kama Insta...
Picha
MAENEO 10 YA KUPUNGUZA MATUMIZI YAKO ILI USEVU PESA NYINGI  Kukata au kupunguza matumizi katika maeneo kadhaa ni mkakati muhimu ambao utakusaidia kuwa na ziada ya pesa kwa ajili ya matumizi mengine muhimu ya kimaendeleo. Tunaangazia maeneo 10 ambayo ukiyazingatia itakusaidia kuwa na kiasi kikubwa cha pesa kinachobakia 1. PUNGUZA MATUMIZI YA KODI YA NYUMBA NA BILI -Pango la nyumba Kama wewe umepanga ni vizuri kuishi nyumba ya gharama nafuu inayoendana na kipato chako ili kupunguza gharama za kulipa kodi kubwa na mwisho wa siku unajikuta pesa yako nyingi inaishia kulipa kodi. Fanya utafiti wa sehemu ambako unaweza kupata nyumba nzuri lakini kwa gharama ya chini ili upunguze gharama za pango. -Bili za umeme na maji Punguza matumizi ya gharama za umeme na maji kwa kuwa na mikakati mbalimbali kama kuzima taa pale ambapo hazitumiki na kutotumia maji hovyo ili kupunguza gharama za umeme na maji. 2. PUNGUZA MATUMIZI YA VYAKULA Chakula ni hitaji la muhimu ambalo kila binadamu anahitaji,na k...
Picha
 FAIDA  ZA KUWA NA TOVUTI (WEBSITE) KWA AJILI YA BIASHARA AU KAMPUNI  Hakuna wakati ambao website ni ya muhimu kama wakati ambapo tupo katika zama za utandawazi. Yawezekana ukajiona kuwa unachofanya ni kidogo hivyo hauhitaji website , hata hivyo kuna mengi utakua unakosa kwa kutokujikita katika kuwa na website kwa biashara au asasi yako. 1) Kukipa thamani ufanyacho Imekua kawaida watu wengi kuamini kuwa biashara au asasi yenye website basi itakua makini . Hata hivyo sio tuu website ili mradi website. Unatakiwa uwe na website ambayo kweli inaonyesha umakini na ubora wa asasi au biashara yako hii inajumuisha website yenye muonekano mzuri, yenye maelezo yaliyokamilika, yenye taarifa ambazo kweli. 2) Kuleta ushawishi Unahitaji website ili kuweza kujenga uaminifu na kuonekana kweli upo serious. Website yako itakupa nafasi ya kuwaeleza watu kwa umakini na kwa ushawishi kile unachofanya  na kwanini wakutafute wewe. Tena website itakusaidia kufanya ushawishi huu kwa watu wen...
Picha
MAKOSA 10 UNAYOFANYA WAKATI WA KUUZA BIDHAA/HUDUMA YAKO NA NAMNA YA KUYAEPUKA Kuuza bidhaa au huduma ni sanaa ambayo lazima ufahamu kanuni zake. Ndio maana wewe na mwenzako mnaweza kuwa mnauza bidhaa au huduma inayofanana lakini mwenzio anauza zaidi ila wewe unaishia kuza kidogo. Kuna baadhi ya makosa ambayo wafanyabiashara wengi wamekua wakiyafanya mara kwa mara lakini hawajui kuwa ni makosa,na huwa yanafanya wasiuze au watumie nguvu kubwa kushawishi mteja. 1.KUTOMSIKILIZA MTEJA VIZURI Hii ni changamoto pale ambapo wewe muuzaji unakua muongeaji kupita kiasi na kutompa mteja nafasi ya kuongea au kuuliza maswali. Kimsingi wewe unatakiwa usiwe muongeaji sana zaidi ya mteja.   Fanya Hivi Tumia muda mwingi kumsikiliza vizuri mteja ana changamoto gani au anahitaji huduma ipi,na wewe jikite kumuuliza maswali machache ili ufahamu shida yake zaidi. 2.KUFOKASI KWENYE MUONEKANO WA BIDHAA BADALA YA FAIDA ILIYOPO Hii imekua changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wengi ambapo wao huzingatia zaidi...